Social Icons

Thursday, March 10, 2011

RAIS JAKAYA KIKWETE AMTEUA SHABANI R.GURUMO KUWA MNIKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Shabani R. Gurumo kuwa Mnikulu (State House Comptroller).

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam,leo,Jumatano, Machi 9, 2011 na Katibu Mkuu Kiongozi, Ndugu Phillemon Luhanjo inasema kuwa uteuzi huo unaanza mara moja.

Kabla ya uteuzi wake,Bwana Gurumo alikuwa Naibu Katibu wa Rais.Bwana Gurumo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Marehemu Rajab Kianda ambaye alifariki dunia Februari 7,mwaka jana,2010.

Mnikulu ndiye msimamizi mkuu na kiongozi wa shughuli zote za nyumbani za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na familia yake, na pia ndiye mkuu wa watumishi wote wanaohusika na shuguli hizo.

Aidha, Mnikulu ndiye msimamizi wa Ikulu na Ikulu Ndogo zote nchini na ndiye hukaribisha mabalozi wapya wanaoziwakilisha nchi zao katika Tanzania wanapokwenda Ikulu kukabidhi Hati za Utambilisho wao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

09 Machi, 201

0 comments: