Social Icons

Tuesday, March 15, 2011

RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI

Rais Jakaya Kikwete (wa pili kulia) akipewa maelezo kutoka kwa Meneja wa Kituo cha huduma za Forodha cha Mamlaka ya Mapato nchini (TRA),Victor Msuya wakati Rais alipofanya ziara kwenye kituo hicho mjini Dar es Salaam.Kulia kwa Rais ni Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya na Kamishna wa Forodha na Ushuru,Walid Juma.
Rais Jakaya Kikwete(wa tatu kushoto)akisikiliza Hotuba ya waziri a Fedha Mustapha Mkulo wakati alipokua akitoa ripoti ya utekelezaji wa mambo mbalimbali ya wizara hiyo.Rais Jakaya Kikwete ametembela Wizara hiyo kwa Mara ya Kwanza Tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwaka Jana
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini Harry Kitiya(kulia)na Gavana wa Benki Kuu Dk Benno Ndulu wakiwa kwenye Mkutano ziara ya fedha na Uchumi leo Jijini Dar es Salaam ambao Rais Jakaya Kikwete aliudhuria
Rais Jakaya Kikwete(kulia)akikaribishwa na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustapa Mkulo Muda Mfupi baada ya Kuwasili Wizarani Hapo Jijini Dar es Salaam Leo
Msemaji wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ingiedi Mduma(mbele) akiwaongoza Kamishna Mku wa Mapato Nchini(TRA) Harry Kitilya(Kulia)na Gavana Mkuu Dk Benno Ndulu Kwenda Kumpokea Rais Jakaya Kikwete leo alipotembelea Wizara ya Fedha na Uchumi Jijini Dar es Salaam
Picha juu ni baadhi ya Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Uchumi wakimsubiri Kumpokea Rais Jakaya Kikwete wakati alipotembelea Wizara hiI leo Jijini Dar es Salaam

0 comments: