Na Ahadi Kakore
Kocha Mkuu wa Simba Mzambia, Patrick Phiri amesema kuwa kiungo wake, Amri Kiemba na mshambuliaji wa Yanga, Davies Mwape ndiyo walikuwa mastaa kwenye mechi ya watani, Jumamosi iliyopita.
Simba na Yanga zilivaana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kutoka sare ya bao 1-1 ambapo Phiri alisema kuwa, wachezaji Kiemba na Mwape ndiyo waliocheza vizuri zaidi.
Akizungumza na Championi Jumatano, Phiri alisema kuwa, ni wazi kwamba wawili hao hawakuwa na mpinzani kwenye mchezo huo kutokana na uwezo mkubwa waliouonyesha kwa dakika zote 90.
“Mechi za Simba na Yanga zinakuwa na hali ya tahadhari kubwa jambo linalofanya hata wachezaji kushindwa kufanya kile walichofundishwa, lakini imekuwa tofauti kwa wachezaji hawa.
“Kila mmoja ameweza kuonyesha kiwango chake chote na nini alichotakiwa kufanya ndiyo sababu mara zote mipira ambayo wamekuwa wakiinasa wanaifanyia kazi.
“Mwape ni mshambuliaji hatari kwa sababu ana nguvu na anatumia akili nyingi na hana maamuzi ya pupa anapokuwa uwanjani. Hii ilichangia kufanya lolote atakalo akiwa ndani ya 18, kitu ambacho kilichangi timu yake kupata penalti.
“Kwa upande wa Kiemba, ni mchezaji mzoefu wa mechi za Simba na Yanga nadhani hilo limechangia kuwa kwenye kiwango kizuri zaidi, lakini achilia mbali hilo, mchezaji huyo ni mmoja kati ya viungo wazuri na wenye kufanya maamuzi ya haraka pale yanapohitajika hasa anapokuwa karibu na lango,” alisema Phiri.
Thursday, March 10, 2011
MWAPE, KIEMBA WAPEWA TUZO
Labels:
www.mateja20.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment