Social Icons

Thursday, March 10, 2011

MEJA JENERALI MSTAAFU,JUMANNE MWAKITOSI AZIKWA DAR ES SALAAM

MAOFISA wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakibeba jeneza lenye mwili wa Meja Jenerali Mstaafu, Jumanne Mwakitosi, wakati wa mazishi yaliyofanyika leo, kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam. Meja Meja Jenerali Mwakitosi alifariki juzi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa
Kisha mazishi kwa mujibu wa dini yake ya Kiislamu yakafanywa. Hapa wahusika wameingia kaburini tayari kuzika.
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Abdulrahman Shimbo (kushoto) akiungana na waombolezaji wengine kuomba dua baada ya mazishi hayo. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Tanga, Meja Jenerali Mstaafu, Saidi Kalembo.
Askari wa JWTZ wakirindimisha mizinga 13 kwa heshima ya kijeshi ya mazishi hayo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uratibu na Bunge, William Lukuvi (kushoto),Waziri wa Ulinzi Dk. Huseein Mwinyi na Waziri wa mambo ya Ndani wa zamani, Lawrence Kego Masha(kulia)walikuwepo kwenye mazishi hayo, bila shaka hapa walikuwa wakiteta jinsi Marehemu alivyokuwa mtu muhimu katika jamii.Picha na Mdau Bashir Nkromo

1 comments:

Desy Ernest said...

mungu amlaze marehemu mahari pema peponi