Baada ya ibada Rafiki wa Karibu na Ndugu wakibeba jeneza la Marehemu kwenda kuzika
Padre Akibariki na Kubatiza Mwili wa Marehemu Mobibo.
Kutoka Kulia Mwenye kiti Wa TA Dr John Lusingu na Mwenyeti wa CCM UK Maina Owino wakiwa katika ibada pamoja na ndugu na marafiki.
Mh Mbunge wa Temeke ABASS MTEMVU na Mke pamoja na watoto wa marehemu wakiweka maua pamoja na mashada kwenye Kaburi la MODIBO
Mke wa marehemu akiweka maua juu ya kaburi la mumewe
Mwenyekiti ya kamati ya msiba Bw SIGSBERT akiwa na mtoto wa marehemu baada ya kuzika.
Mamia ya Waombelezaji wakiwa makuburini
----
MATEJA20 inawaletea Matukio katika picha ya Kumuaga Marehemu MODIBO KEITA DENISS mjini Manchester UK. Leo Jumatano 16.3.10 ndugu, marafiki na jamaa walijumuika katika kanisa la OUR LADY'S CHURCH huko Manchester kwenye Ibada iliyofanyika ya kumuombea na kumwaga marehemu. Baada ya huduma ya kanisa umati wote ulieleka Makaburini kwa ajili ya Maziko. Watu mbalimbali walijitokeza leo akiwepo kaka wa marehemu Mbunge wa Temeke MH ABBASS MTEMVU , mwenyekiti wa TANZ UK JOHN LUSINGU, MWENYEKITI WA CCM UK MAINA OWINO, JUMUIYA YA KISOMALI Na mataifa mengine.

Marehemu MODIBO atakumbukwa na wengi kwa jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kwa kujitolea kwake mhanga kwa ajili ya kusaidia wengine, hayo yalisemwa na watu mbali mbali kuanzia watoto pamoja na mataifa mengine mara baada ya kuzika katika hafla fupi ilioandaliwa na wanakamati. Hivyo Basi kwa kumuenzi marehemu Jumuiaya ya kitanzania Manchester imeahidi kuendeleza yale yote mema aliyoanzisha na kuwahamasishwa wengine. Mwisho kwa Niaba ya Familia na rafiki wa marehemu inapenda kutoa shukrani zao za dhati kwa wale walijitolea kusaidia kwa namna moja au nyingine wakati wa kumuuguza marehemu na kufanikisha shughuli ya leo. Mungu awabariki wote.
ASANTENI
0 comments:
Post a Comment