Social Icons

Thursday, March 10, 2011

B 12 MIKONONI MWA POLISI

Na IDDY HAMISY
Presenta wa Kituo cha Redio cha Clouds FM, Khamis Mandi ‘B12’ (pichani), ameingia kwenye mtiti na polisi wa usalama barabarani.

Mtangazaji huyo anayejulikana pia kama ‘The King of Afternoon Show’ alidakwa na ‘trafiki’ hao katika Makutano ya Barabara ya Kawawa na Ali Hassan Mwinyi kwenye mataa ya Morocco, Dar kwa makosa ya kutofuata ruhusa ya taa na kutofunga mkanda.

Ilielezwa kuwa, akiwa na haraka ya kuwahi muda wa kipindi chake cha XXL, B12 alipita kwa kasi licha ya kuwa tayari taa hizo zilikuwa zimeashiria kusimama bila kujua kuwa mbele kulikuwa na askari aliyekuwa amesimama kuangalia usalama sehemu hiyo.

“Unajua jombaa sikujua kama kuna askari mbele, nimekuja spidi nawahi `time` ya XXL, kimtindo niliamini naweza kuwahi taa lakini hesabu zikawa siyo, nikaamua kupita hivyo hivyo ndiyo unaona afande kanikamata,” alisema B12 baada ya kuulizwa yaliyomkuta.

Hata hivyo, msala wa mtangazaji huyo ulimalizika dakika sifuri baada ya kulipa faini ya shilingi elfu arobaini za Kibongo na kuwasha gari lake aina ya Toyota Cresta GX 110 nyeusi na kusepa kwa kasi kuwahi kipindi.


0 comments: