Na Shakoor Jongo
Mhusika katika kiwanda cha filamu Bongo, Rose Ndauka (pichani), amefunguka kuwa, waigizaji wenzake wana tabia za kishirikina hivyo hawezi kufanya kazi na watu wa aina hiyo.
Akizungumza na Amani Jipya jijini Dar juzi, Rose alisema kuwa, hivi karibuni kumeibuka tuhuma kwa baadhi ya waigizaji kudaiwa kujihusisha na mambo ya kishirikina kitu ambacho si kizuri na kinaharibu sifa ya tasnia hiyo.
Alisema wasanii hao wanapaswa kutambua kuwa, wakitegemea sana mambo ya kishirikina, mwisho watakuwa wanajiamini na kulipua kazi hivyo kujishusha mbele ya jamii.
“Tuhuma za ushirikina kwa baadhi ya wasanii zinaniumiza sana, hasa pale ninaposikia wengi wao wanaojihusha na mambo hayo ni walimu wangu kwenye tasnia hii ya uigizaji.
“Wanafanya hivyo ili nyota zao ziwe juu huku wakiwafunika wenzao kwa kutumia makafara,” alisema Rose na kuongeza:
“Mimi hilo sikubaliani nalo kabisa, juhudi za mtu katika utendaji wake wa kazi ndiyo utamfanya kuwa juu zaidi na si kwenda kwa waganga, nikigundua kuwa hawa mastaa wenye majina makubwa ndiyo wanaojihusisha na imani hizo za kishirikina, kiukweli nitaepukana nao, hata nikiitwa kufanya nao kazi sitakuwa tayari.”
Hivi karibuni kumekuwa na tuhuma za ushirikina zinazovurumishwa kwa baadhi ya wasanii wenye majina jambo linaloleta picha ya tofauti miongoni mwa wadau wa filamu nchini.
0 comments:
Post a Comment