Social Icons

Saturday, March 12, 2011

AKODI WAPAMBE...


Na jeffrey evarist

Ama kweli Jiji la Dar es Salaam lina mambo! Mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Adella, mkazi wa Mburahati, Dar amekodi wapambe kwa ajili ya kwenda kumchukua mumewe kwa hawara.

Kituko hicho cha mwaka kilichofuatiliwa hatua kwa hatua na Risasi Jumamosi, kilijiri maeneo ya Biafra Kinondoni ambapo Adella, akiwa na wanawake kadhaa, walivamia nyumbani kwa mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Rahma kwa madai ya kutaka amwachie mumewe.

Adella alidai kuwa, mumewe (hakutaka kumtaja jina) amekuwa ‘mwingi wa habari’ hivyo anaamini kwamba Rahma ambaye pia ni mke wa mtu ndiye anayemwibia ‘mali’ zake.

AKODI WAPAMBE
Mwanamke huyo alidai kuwa, alitonywa na ‘wanamtandao’ wake kwamba Rahma amekuwa ‘akitoka’ na mumewe, hivyo akaamua kukodi wapambe na kwenda kumvamia ili kumshikisha adabu mbele ya mumewe.

Adella na ‘mashostito’ wake walipanga mikakati kabambe huku wakijiweka sawa kwa lolote litakalotokea ambapo walizama nyumbani kwa Rahma lakini bahati haikuwa upande wao kwani hawakumkuta ‘mbaya’ wao.
WAPAMBANA NA ‘HAUSIGELI’

Katika hali ya aina yake, Adella na wapambe wake walimvaa mfanyakazi wa ndani ‘hausigeli’ wa Rahma na kumtaka aeleza alipo bosi wake la sivyo wangemlipua na mabomu kama yale ya Gongo la Mboto.

Mfanyakazi huyo aliwaambia kuwa bosi wake alitoka dakika chache kabla ya wao kufika, hivyo akawataka wamuibukie jioni.

Baada ya kumkosa ‘mtuhumiwa’, waliondoka nyumbani hapo huku wakimtaka hausigeli kumfikishia taarifa bosi wake kuwa wanamsaka.
Kama ilivyo ada ya Risasi Jumamosi, lilimvuta pembeni Adella ili kusimulia mkanda mzima wa mkasa huo.

Hata hivyo, Adella hakutaka kuanika ishu kamili kwa maelezo kwamba ataharibu mipango ya kumnasa Rahma lakini akaahidi kufanya hivyo baada ya kukamilisha zoezi lake.

Alisema: “Hii ni Vita Kuu ya Tatu ya Dunia. Sitaki kuvujisha mchongo kwani nitaharibu mikakati ya kumnasa mbaya wangu.
“Nimepanga kumshikisha adabu ili atambue kwamba mume wa mtu ni sumu.”
Jitihada za kumpata Rahma kuzungumzia mkasa huo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kutokuwa hewani.

0 comments: