Miriamu akiwaelezea waandishi wa habari jinsi uzinduzi wake utakavyokuwa.
MUIMBAJI wa nyimbo za injili nchini, Miriamu Lukindo leo amefanya mkutano na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari katika Mgahawa wa Hadees uliopo Posta jijini Dar es Salaam, akiwaeleza maandalizi ya uzinduzi wa albamu yake aliyoipa jina la Ni Asubuhi.
Miriamu amesema uzinduzi huo utakafanyika Aprili 10, 2011 ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Miriamu akiwa pamoja na Mratibu wa tamasha lake, John Momadi ( wa kwanza kulia) pamoja na Meneja wake, Humphery Maziba wakiwa tayari kwa ajili ya kuongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi huo.
Mratibu wa uzinduzi huo, John Momadi akizungumza jambo.
Miriamu akiwa na kamati ya maandalizi ya uzinduzi huo.
Stori/Picha: Imelda Mtema / GPL
0 comments:
Post a Comment