Social Icons

Monday, December 27, 2010

CHEKI MAMBO YALIVYOJIRI X-MAS


JANA usiku mtandao wako ulitembelea katika kumbi mbili tofauti, za PTA uliyopo ndani ya viwanja vya Sabasaba jijini Dar ambako kulikuwa na onyesho la bendi inayocheza muziki wake kiasili zaidi, Makhirikhiri kutoka Botswana. Baada ya hapo kamera yetu ilijimuvuzisha maeneo ya Msasani katika ukumbi wa Msasani Club ambako kulikuwa na onyesho la bendi ya Taarabu ya Five Star.Pichani ni dada mmoja ambaye alionekana kukolea kwa kilaji akiwa amevamia jukwaa la waimbaji wa bendi ya Five Star na kuserebuka huku akiwa amemshikilia mmoja wa waimbaji hao.


Mashabiki wa taarabu wakijimwayamwaya katika onyesho hilo.


Kundi la Makhirkhiri likifanya vitu vyake Ukumbi wa PTA jana


Mmoja wa wanamuziki hao wa Makhirikhiri akicheza staili ya Kibajaji

0 comments: