Social Icons

Thursday, November 11, 2010

TOXSTAR KUDONDOKA NA ALBAMU


MSANII wa muziki wa Kizazi kipya Bongo anayetokea katika lebo ya Shalobaro Records Juma Said ‘Toxstar’juzikati ameibuka na kudai kuwa amekamilisha maandalizi ya albam yake mpya ambayo hakuitaja kwa jina kutokana na sababu zake maalum.

Toxsta alipiga stori hizo na Mateja20 baada ya kukutana nae mitaa ya Sinza Jijini Dar es Salaam Novemba 11 mwaka huu ambapo alikuwa katika mishemishe za kukamilisha wimbo wake mpya utakao itamburilsha albam hiyo.

Toxstar alisema kwamba kabla ya kutoa albam hiyo ataachia single mpya ambayo ni Remix ya wimbo wa Pretty Girl aliyowashirikisha wasanii mbalimbali wa Bongo flava kama Ali Kiba,Ngwea,God Zilah na Udauda, ataiachia hewani kuanzia wiki ijayo ikiwa kwenye Audio na Video.

Toxstar aliongeza kuwa albam hiyo itakuwa na jumla ya nyimbo 10 ambazo ni Petty Girl,Petty Girl Remix,Candle Light, Naomba Nielewe,Sisemi,Best Friend, One Two na My Life.

Alitumia flusa hiyo kuwaomba mashabiki zake wote wakae mkao wa kupokea albam hiyo ambayo imesheheni vigongo vikali na kwamba itakuwa na ladha za kimataifa zaidi.


0 comments: