KUNDI la muziki la Top Band inayomilikiwa na Khaleed Mohamed ‘TID’ usiku wa kuamkia leo ilifanya shoo ya uhakika ndani ya ukumbi wa Billicanas Club jijini Dar es Salaam ambapo ilihudhuriwa na kundi la wanamuziki wa ‘Mapacha Watatu’ ambao pia walipata nafasi ya kutumbuiza kwa kibao chao cha ‘Kuachwa’.
Akiongea na paparazzi wetu ndani ya klabu hiyo, TID alisema kwamba bendi hiyo itakuwa ikifanya shoo zake kila siku ya Jumanne ndani ya ukumbi huo hivyo aliwaomba mashabiki wake waendelee kumsapoti kila ifakapo siku hiyo.
0 comments:
Post a Comment