Social Icons

Wednesday, September 8, 2010

P DIDY WA MAIMARTHA AFARIKI DUNIA

PERFECT KAGISA 'P DIDY'
HABARI ZILIZOTUFIKIA MUDA HUU, ZINASEMA KWAMBA MKURUGENZI MSAIDIZI WA BENDI YA MUZIKI WA DANSI YA DIAMOND MUSICA, PERFECT KAGISA 'P DIDY' AMEFARIKI DUNIA. INAELEZWA P DIDY AMEFARIKI GHAFLA BAADA YA KUANGUKA, BARABARA YA LUMUMBA, MNAZI MMOJA, JIJINI DAR ES SALAAM ALIPOKUWA KATIKA MIZUNGUKO YAKE. "NI KWELI AMEANGUKA MBELE YA MACHO YANGU," ALISEMA MMOJA WA MASHUHUDA WA TUKIO HILO. NAYE MTANGAZAJI WA KITUO CHA RUNINGA CHA TBC 1 CHA JIJINI DAR, ANAYETANGAZA KIPINDI CHA B&M BENNY KINYAIYA ALIUELEZA MTANDAO HUU KUWA: "NI KWELI, NIPO MUHIMBILI MUDA HUU." BEN HAKUWEZA KUZUNGUMZA ZAIDI KWANI ALIKUWA AKILIA MUDA WOTE ALIOKUWA AKIHOJIWA NA MATEJA20. TUNAENDELEA KUFUATILIA TAARIFA HII KWA UKARIBU NA TUTAWALETEA KILA KINACHOJIRI. - Mateja20.


Baadhi ya ndugu wakiwa msibani

Wakilia kwa machungu.
Baadhi yao wakiwa hoi.
Ndugu na jamaa wakimpa moyo Maimartha.
Pole Mai kwa makubwa haya.
Mungu alitowa bwana ametwaa, Jina lake libarikiwe.

0 comments: