Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Utamaduni cha Ufaransa, Didier Martin (katikati) akiwasilisha mada yake iliyohusu mchango wa asasi kama yake katika kukuza sanaa na utamaduni wa Mtanzania. Kushoto kwake
ni Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego na Ruyembe Mulimba.

KITUO cha Kimataifa cha Utamaduni cha Ufaransa (Alliance Française) kimewataka wasanii wa Bongo kutumia programu yake ya ‘Barazani’ katika kutangaza kazi zao na kuzifanya zitambulike na kupata soko kimataifa.
‘Barazani’ ni programu ya ‘pafomansi’ za kisanaa ambayo imekuwa ikiwahusisha wasanii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na imekuwa ikifanyika kwa mwezi mara moja kwenye kituo hicho. Mwezi huu itafanyika tarehe 15.
Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwa kuandaliwa na BASATA likishirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz), Mkurugenzi wa Kituo hicho Bw. Didier Martin, alisema wasanii hawana budi kulitumia jukwaa hilo katika kuuza na kutambulisha kazi zao kwani limekuwa likihudhuriwa na watu mbalimbali kutoka sehemu tofauti duniani.
Aliongeza kwamba ushiriki wa wasanii kwenye jukwaa hilo uko wazi na kinachotakiwa ni wasanii wenyewe kuchangamkia fursa hiyo kwa kufika kwenye kituo hicho na kujiandikisha.
Aidha, alisema kwamba, kwa sasa kituo hicho kinatoa mafunzo ya lugha ya Kifaransa kwa watu mbalimbali na kuongeza kwamba, gharama za malipo zimepunguzwa kwa wasanii hadi kwa zaidi ya asilimia hamsini hivyo ni fursa pekee kwa wasanii kujifunza lugha hiyo ya kigeni.
Kuhusu nyimbo za wasanii wa muziki kusikika redioni, alisema kwamba, Ufaransa imefungua kituo cha redio ambacho kitarusha matangazo kwa lugha ya Kiswahili na kuongeza kwamba, mwezi ujao wanatazamia kuanzisha dawati la Kiswahili hivyo kutoa fursa kubwa kwa wasanii wote.
Masuala mengine ya msingi yaliyojadiliwa kwenye jukwaa hilo ni pamoja na haja ya kituo hicho kupenya hadi vijijini, kusaidia kuhamasisha wawekezaji wa Kifaransa kujenga studio za kurekodia nchini, kusaidia usambazaji wa kazi za wasanii, kutoa misaada ya kifedha kwa wasanii nchini, kuzitangaza kazi za wasanii wa ndani nje ya mipaka, n.k.
Akijibu masuala hayo, Martin alisema kwamba, kwa sasa kituo chake kinatoa msaada wa fedha kwa wasanii wanaofanya sanaa zenye uasili wa Tanzania na kusisitiza kwamba, wasanii wa Tanzania lazima waachane na dhana ya kunakiri kazi kutoka nje bali wajikite kwenye kutengeneza kazi za sanaa za asili.
Aliongeza kwamba, tatizo la masoko ya kazi za sanaa ni kubwa lakini akasisitiza kwamba, wasanii wanapaswa kujikita kwenye ubunifu wa kazi zilizo bora na zenye kubeba asili ya Tanzania ili kuzifanya kuwa tofauti na zile zinazotolewa sehemu zingine duniani.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonce Materego, alisema kwamba, baraza lake litaendelea na utaratibu wa kuwapa wasanii fursa mbalimbali za kukutana na wadau wa sanaa wa ndani na nje. Pia alikumbusha kitu ambacho muda wote amekuwa akikisisitiza, yaani wasanii wetu kubuni kazi zenye asili ya kwetu.
Alisema kwamba, kunakiri kila kitu kutoka nje maana yake ni kudumaza sanaa yetu na hivyo kuwafanya wasanii kushindwa kushindana kwenye masoko kutokana na kutengezeza kazi zinazopatikana kwingineko duniani.

Msanii wa kizazi kipya, Symon John aka Gheto King, akichangia hoja.
“Saidieni jamani sanaa yetu ikue,” ndivyo Mzee Rashid Masimbi ambaye ni mtaalamu wa sanaa za maonyesho alivyokuwa akitoa mchango wake.
Sehemu ya wadau wa Jukwaa la Sanaa wakifuatilia kwa makini wasilisho la Didier Martin.
Mkongwe wa muziki wa dansi, Hussein Jumbe, yeye alitaka aelezwe ni kwa jinsi gani ataweza kushiriki Tamasha la Sauti za Busara ambalo limekuwa likidhaminiwa pia na kituo hicho.
Ghonche Materego (kushoto) akibadilishana mawazo na Didier Martin, muda mfupi baada ya kuahirisha hafla hiyo hadi Jumatatu ijayo ambapo mada kuhusu Changamoto za Sanaa ya Unenguaji itawasilishwa.
0 comments:
Post a Comment