STL & AY
Wednesday, December 28, 2011
STL & AY
MBUNGE WA WAWI, HAMAD RASHIDI MOHAMMED AIVIMBISHIA MSULI CAFU
MBUNGE wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed (CUF) ameigomea Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho kumhoji na kumjadili kuhusu tuhuma zinazomkabili za kukiuka Katiba, akidai hana imani na wajumbe wake.
MKESHA WA KULIOMBEA TAIFA KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA DESEMBA 31 MWAKA HUU
Umoja wa makanisa ya Kikiristo Tanzania (Tanzania ChristianFellowship of Churches) umeandaa mkesha mkubwa kwa ajili ya dua maalum kwa taifa kwa lengo la kumshukuru Mungu kwa kulivusha taifa katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru na kuanza kipindi kingine ambapo mgeni rasmi katika mkesha huo atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Mkesha mkuu kutoka Tanzania Christian Fellowship of Chrches Askofu Godfrey Emmmanuel Malasi amesema watanzania wanapaswa kujua Mungu anakusudi gani na taifa la Tanzania katika kipindi hiki ambacho Taifa limetimiza miaka 50 ya uhuru na kuanza kipindi kingine na kutoa wito kwa kila mtanzania kufanya kazi kwa bidii na kushiriki katika uchumi wa taifa.
Amesema serikali inazo sera nzuri za kuweza kuwamilikisha wananchi rasilimali ziliizopo nchini ili waweze kuishi maisha bora na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kutambua majira na wakati uliopo sasa wakati taifa linapoanza miaka 50 mingine ya uhuru kwa kuzitumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo.
“Kila mmoja anapaswa kushiriki na kushirikishwa kikamilifu katika uchumi wa taifa letu ambalo sasa limemaliza miaka 50 ya uhuru, kila mtu anapaswa kutambua nafasi yake, tusikae kwa kubweteka, tusikae kwa kulalamika kila mtu ajue ni wakati wa kumiki na kurithishwa rasilimali zilizopo katika taifa hili”
Amesema mwaka huu dua maalum kwa taifa litafanyika katika mikoa 14 ya Tanzania ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza,Kilimanjaro, Singida Iringa, Mbeya ,Iringa, Kagera, Dodoma, Ruvuma, Tabora,Tanga na visiwa vya Zanzbar na Pemba.
Amefafanua kuwa katika mkesha huo viongozi mbalimbali wa taifa ,vyama vya siasa na balozi mbalimbali zipatazo 37 zilizopo nchini zimearikwa kushiriki mkesha huo na kuongeza kuwa tayari baadhi ya balozi zimethibitisha kushiriki mkesha huo.
Kuhusu maadalizi ya mkesha huo askofu Godfrey Malasi amesema yanaendelea vizuri na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika dua hiyo maalum na kuongeza kuwa mkesha huo utaambatana na tukio maalum la watoto 50 kusimama uwanjani na kutamka maneno ya kupokea miaka 50 ijayo ikiwa ni ishara ya kupokea kizazi huru cha watanzania.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati ya mkesha mkuu wa Taifa Askofu Keneth Damas ameipongeza serikali kwa kuwa na msimamo wa kupinga suala la ndoa za jinsia moja (ushoga) katika mikutano ya kimataifa iliyofanyika hivi karibuni na kuuita uamuzi huo kuwa ni ushindi mkubwa kwa taifa la Tanzania na watu wake katika kuheshimu utu na utamaduni wa taifa na uukataaji wa vitendo vya udhalilishaji na kuongeza kuwa wao kama viongozi wa dini wataendelea kuonya na kufundisha watu wajue athari za dhambi hiyo.
Habari: Aron Msigwa/MAELEZO
KAFULILA KUENDELEA NA UBUNGE FEBRUARI 2012
MAHAKAMA Kuu Dar es Salaam, imeamuru Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, kuendelea na wadhifa wake wa ubunge hadi hapo kesi yake ya msingi itakaposikilizwa
Hivi karibuni, Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi, ilimfukuza Kafulila uanachama, uamuzi ambao unamuondolea sifa ya kuwa mbunge.
Hata hivyo, kutokana na uamuzi wa Mahakama Kuu leo, Kafulila ataendelea kushikilia nafasi yake ya ubunge mpaka hapo kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa hukumu.
Uamuzi huo wa mahakama, umefuatia kesi iliyofunguliwa na Kafulila, kupinga uamuzi wa Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi wa kumvua uanachama na kumuondolea sifa ya kuendelea kuwa mbunge.
Kafulila alipozungumza na mwandishi wetu alisema kuwa Mahakama Kuu itakaa Februari mwakani na kupanga kuanza kusikiliza kesi hiyo.
“Namshukuru Mungu, siku zote Mungu yupo pamoja na wanyonge. Bado nasimamia ukweli kwamba kikao cha Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi kilichoamua, kilikiuka sheria na taratibu. Hata hivyo, suala hili lipo mahakamani, tuache mahakama itaamua,” alisema Kafulila.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, amepongeza uamuzi wa mahakama na kueleza kwamba ni mpango wa Mungu kumtetea mnyonge.
Zitto, aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii, Facebook leo saa 9:40 alasiri: “Kafulila kuendelea na ubunge. Mahakama Kuu imetoa amri muda mfupi uliopita. Ataendelea kuwa mbunge mpaka hapo kesi ya msingi itakapokwisha. Mungu yupo pamoja na wanyonge.
Na Sufianimafoto Blog
Tuesday, December 27, 2011
MADIWANI FUATILIENI MIRADI YA MAENDELEO
Na Gladness Mushi, ARUSHA
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Magesa Mulongo,amesema kuwa kama madiwani kutoka katika kata zote watashiriki katika kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo ya vijiji na kata basi miradi hiyo itaweza kujengwa katika viwango vya hali ya juu sana na pia itaweza kuwanufaisha zaidi wananchi ambao ndio walengwa wa miradi hiyo.
Bw Magesa aliyasema hayo hivi karibuni mkoani Arusha wakati akiongea na viongozi mbalimbali wa serikali za mitaa kuhusu masuala na mikakati mbalimbali ya kimaendeleo kwa Mkoa wa Arusha.
Amesema,ili miradi iboreshwe kwa kiwango ambacho kinakubalika ni lazima kuwe na mipango mahususi kwa viongozi wa serikali hizo hasa Madiwani ambapo wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa wasimamizi wazuri wa miradi ambayo inalenga kutoa huduma kwa jamii.
Alisema kwa utaratibu huo wa kufuatilia na kukagua mara kwa mara shuguli za miradi hiyo ya maendeleo katika ngazi ya kata unawezekana kufanyika na kuwa na manufaa kwa wananchi ambapo ufuatiliaji huo unaweza kuungwa mkono hata na ngazi ya halmashauri.
Alibainisha kuwa ni wazi miradi mbalimbali katika ngazi za kata,Vijiji,zinashindwa kukamilika na kuwafikia watumiaji ambao ndio waliolengwa, kwa kuwa bado baadhi ya watendaji wanashindwa kufuatilia kwa ukaribu miradi hiyo hali ambayo inasababisha hasara kubwa sana kwa Serikali, na Wahisani mbalimbali.
“Nawasihi sana Madiwani hakikisheni kuwa mnajua na kufuatalia miradi yote ambayo imo kule kwenye kata zenu hata kama miradi hiyo si ya Serikali kwa kuwa malengo halisi ya miradi hiyo ni kumkomboa Mtanzania”alisema bw Magesa.
Akizungumzia suala la usimamizi wa Fedha alisema kuwa nao maafisa mipango wanatakiwa kuhakikisha na kukagua ubora wa mradi kabla hawajapitisha malipo mbalimbali kwa ajili ya miradi hiyo kwa kuwa baadhi ya miradi inapitishwa na halmashauri wakati miradi hiyo haina ubora uliokusudiwa.
“Eti unakuta mkuu wa idara anakaa ofisini alafu anapitisha malipo
kwa ajili ya miradi wakati hajui hata mradi ulipo,wala ubora wake sasa watu wa hali hii mimi sitawaacha kabisa na badala yake nawasihi sana madiwani kuwa hakikisheni kabla hamjapitisha mradi mnashirikiaana na halmashauri zenu hata kwa njia ya ushauri wa wataalamu wake’aliongeza Bw Magesa.
Aliwataka wakuu wa idara kuhakikisha kuwa wanashirikiana na uongozi mbalimbali wa serikali za vijiji katika kuboresha na kuimarisha miradi ya Serikali pamoja na Miradi ya wahisani ili kuharakisha maendeleo kwa walengwa hasa katika maeneo ya vijijini.
Habari/Picha: Fullshangwe Blog
WATANZANIA TUENDELEE KUWACHANGIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO
Monday, December 26, 2011
Rapa machachari wa Bendi ya African Stars International 'Twanga Pepeta', Msafiri Diouf akikamua mbele ya mashabiki zake katika shoo maalum ya sikukuu ya Krismasi iliyofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mpiga Dramu mkuu wa bendi hiyo, James Kibosho akiwajibika kwenye onesho hilo.
Mpiga solo mkongwe wa bendi hiyo Miraji Shakashia 'Shaka Zoru' (kushoto), akipiga gitaa huku akiunda pozi na shabiki wake namna hiyo.
Staa wa bendi hiyo Charles Gabriel 'Chalz Baba' (kulia mbele), akicheza kwa pamoja na wanenguaji wa bendi hiyo.
Muimbaji machachari wa bendi hiyo Dogo Rama, akicheza kwa staili yake huku akiwa amembeba mmoja wa wanenguaji wa bendi hiyo Mary Hamisi.
Dogo Rama akikatika kwa staili yake na Maria Soloma.
Mnenguaji wa Bendi hiyo Asha Saidi 'Sharapova' akiwajibika mbele ya mashabiki zake.
Wanenguaji wa kiume wa bendi hiyo wakiwajibika jukwaani hapo.
Baadhi ya mashabiki wa bendi hiyo wakishuhudia kwa makini zaidi burudani zilizokuwa zikitolewa Ukumbini hapo.



