MKESHA WA KULIOMBEA TAIFA KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA DESEMBA 31 MWAKA HUU
Umoja wa makanisa ya Kikiristo Tanzania (Tanzania ChristianFellowship of Churches) umeandaa mkesha mkubwa kwa ajili ya dua maalum kwa taifa kwa lengo la kumshukuru Mungu kwa kulivusha taifa katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru na kuanza kipindi kingine ambapo mgeni rasmi katika mkesha huo atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Mkesha mkuu kutoka Tanzania Christian Fellowship of Chrches Askofu Godfrey Emmmanuel Malasi amesema watanzania wanapaswa kujua Mungu anakusudi gani na taifa la Tanzania katika kipindi hiki ambacho Taifa limetimiza miaka 50 ya uhuru na kuanza kipindi kingine na kutoa wito kwa kila mtanzania kufanya kazi kwa bidii na kushiriki katika uchumi wa taifa.
Amesema serikali inazo sera nzuri za kuweza kuwamilikisha wananchi rasilimali ziliizopo nchini ili waweze kuishi maisha bora na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kutambua majira na wakati uliopo sasa wakati taifa linapoanza miaka 50 mingine ya uhuru kwa kuzitumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo.
“Kila mmoja anapaswa kushiriki na kushirikishwa kikamilifu katika uchumi wa taifa letu ambalo sasa limemaliza miaka 50 ya uhuru, kila mtu anapaswa kutambua nafasi yake, tusikae kwa kubweteka, tusikae kwa kulalamika kila mtu ajue ni wakati wa kumiki na kurithishwa rasilimali zilizopo katika taifa hili”
Amesema mwaka huu dua maalum kwa taifa litafanyika katika mikoa 14 ya Tanzania ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza,Kilimanjaro, Singida Iringa, Mbeya ,Iringa, Kagera, Dodoma, Ruvuma, Tabora,Tanga na visiwa vya Zanzbar na Pemba.
Amefafanua kuwa katika mkesha huo viongozi mbalimbali wa taifa ,vyama vya siasa na balozi mbalimbali zipatazo 37 zilizopo nchini zimearikwa kushiriki mkesha huo na kuongeza kuwa tayari baadhi ya balozi zimethibitisha kushiriki mkesha huo.
Kuhusu maadalizi ya mkesha huo askofu Godfrey Malasi amesema yanaendelea vizuri na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika dua hiyo maalum na kuongeza kuwa mkesha huo utaambatana na tukio maalum la watoto 50 kusimama uwanjani na kutamka maneno ya kupokea miaka 50 ijayo ikiwa ni ishara ya kupokea kizazi huru cha watanzania.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati ya mkesha mkuu wa Taifa Askofu Keneth Damas ameipongeza serikali kwa kuwa na msimamo wa kupinga suala la ndoa za jinsia moja (ushoga) katika mikutano ya kimataifa iliyofanyika hivi karibuni na kuuita uamuzi huo kuwa ni ushindi mkubwa kwa taifa la Tanzania na watu wake katika kuheshimu utu na utamaduni wa taifa na uukataaji wa vitendo vya udhalilishaji na kuongeza kuwa wao kama viongozi wa dini wataendelea kuonya na kufundisha watu wajue athari za dhambi hiyo.
Habari: Aron Msigwa/MAELEZO
1 comments:
Kiongozi kapewa majukumu ya kuandaa na kusaini mikataba kwa manufaa ya umma, lakini kachukua 10%, labda kaagiza vipuri, kachukua mgao na kaleta vipuri vibovu, kadai maposho yasioeleweka, kasimamia miradi, ila hakuna kilichofanyika na kala hela zote, na ikatokea hata jela hajaiona, sasa mwenyezi mungu atakusaidia nini hapo????
Acheni kupoteza muda wetu na maombi yenu yasio na kichwa wala miguu.
Swala ni sheria za nchi hazichui mkondo wake, period.
Hakuna cha maombi wala nini hapo!
Post a Comment