YOUNG
Na Erick Evarist
Bwa mdogo anayefanya poa kunako gemu la Hip Hop Bongo, Young Dee, amefunguka kuwa siku si nyingi atamuanika peupe demu wake.
Akichonga na MATEJA20 kwa njia ya simu Young Dee, amesema tamaduni za kiafrika ndiyo kitu pekee kilichokuwa kikimfanya ashindwe kumuanika mpenzi wake lakini siku si nyingi atamuweka wazi kwani kwa sasa umri wake utakuwa unamruhusu kufanya hivyo.
“Mi nina miaka 19 kwa sasa na kusema kweli mpenzi ninaye toka kitambo na siku si nyingi nitamuanika tu kwa mashabiki wangu ingawa kwa upande mwingine nahofia inaweza kuwa ni msala mkubwa kwao maana siku zote huwa najua tabia za wabongo katika suala hili kuna kumkubali au laa na ikaleta madhara hadi kwenye game yangu,” alisema Young Dee.
Young Dee pia alifunguka juu ya tamaduni za kitanzania kwa kudai ingekuwa ni nchi za mbele ilikuwa ni rahisi kujiachia na kiburudisho chake kila sehemu kama ilivyo kwa msanii mdogo wa kimarekani, Justine Bieber na mpenziwe Selena Gomez.
“Pamoja na hayo yote muda mwingine nakuwa nahisi kama wadau wangu hawatanielewa vibaya sababu mimi sitakuwa wa kwanza kufanya hili kwa wanamuziki hapa duniani kwani mfano mzuri utabaki kuwa kwa msanii mwenye umri mdogo
“ So kutokana na hili naomba wadau wangu wote nitakapo fikia uamuzi huu wasije kunitenga na kuniona tofauti kwani
Je, wadau wa Mateja20 mnasemaje kuhusiana na hili suala la bwana mdogo Young Dee kuweka kiburudisho chake kweupe, ebu toweni maoni yenu ili kumweka sawa dogo asije akajikuta anapotea.
3 comments:
daaaaaaaaaaaa......co inshu mdogo wng kwanza umekaza kinoma...me mwenyewe nlikua na hyo k2 since std 6 mpaka ss nko univazty ila kuwa mwaminif........
daaaaaaaaaaaa......co inshu mdogo wng kwanza umekaza kinoma...me mwenyewe nlikua na hyo k2 since std 6 mpaka ss nko univazty ila kuwa mwaminif........
Mmh.yale yale ya diamond na wema
Post a Comment