Social Icons

Wednesday, September 14, 2011

KWAHERI UMASIKINI, KARIBU TUJIKOMBOWE!!!
KAMPUNI ya Dimond Integrated Solution and Awareness, imeandaa Tamasha kubwa litakalo kutanisha watu zaidi ya elfu mbili katika Viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mateja20, Leo Mratibu wa Tamasha hilo,Mahmoud Omar, amesema kwamba tamasha hilo litakuwa na lengo la kuelimisha vijana na watu wa lika mbalimbali ili kuwapa njia za kuwa wajasiriamali.

Mahmoud alisema kwamba, tamasha hilo litachukuwa la siku mbili, Septemba 15-16 mwaka huu na mafunzo yatakayotolewa ni pamoja na kutengeneza sabuni za miche na maji, shampoo, mishumaa, mafuta ya kupaka, Lotion, maji ya battery, Tomato source, Chilli source, Unga wa lishe Wine aina zote, biskuti, keki, Juice aina zote, ufugaji na kutengenmeza vyakula vya mifugo na biashara kwa ujumla.

Ada ya masomo yote itakuwa sh. 30,000/= kwa masomo ya nadharia na vitendo. Muda kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 12:00 mchana kasha mafunzo yataendelea saa 8: 00 alasiri hadi saa 12: 00 jioni.

Karibu tushirikiane kuondoa umasikini Tanzania, Ewe mwananchi wa Dar es Salaam.

0 comments: