KUNDI JIPYA LA MUZIKI WA GOSPEL KUINGIA KITAANI
WAPENZI wa muziki wa injili Bongo, mnatakiwa kukaa mkao wa kupokea kundi jipya la muziki wa injili linalotarajiwa kuanza kazi zake za kumuhubiri kristo hivi karibuni, Kundi hilo litaongozwa na warembo wawili ambaye ni Jessica Honore, ambaye nyota yake uimbaji inamulika kisawasawa pamoja na Angel Bernard, ambaye amepata kutamba na wimbo wa Yote yalikwisha pale msalabani baba nashukuru asante
Jessica na Angel wakiwa katika pozi
Mwanzilishi wa kundi hilo ni Jessica ambaye aliamua kumshirikisha mwanadada mwenzie na kwamba kundi hilo litafahamika kwa jina la LEVITICUS DIVAS likiwa na lengo la kumtangaza kristo, wadada hawa wamesema wameamua kuwa na kundi hilo baada ya kuona huduma ya kumtangaza kristo haijafikiwa kiumakini zaidi na makundi mengi yanayofanya muziki wa gospel, wamesema kundi lao litagusa jamii kwa ujumla na maisha ya kila siku kwakuwa waimbaji waliowengi hawazitumii nafasi zao kisawasawa
Jessica akimtukuza Mungu katika jukwaa la CCC Upanga
Pamoja na kuanzisha kundi hilo Jessica pia anashiriki katika kundi la Next level lenye makazi yake katika kanisa la Tanzania Assemblies of God (ccc) Upanga ambapo uimbaji wake unawabariki wengi ambapo wamekuwa wakimtaja kuwa kiwango chake kipo katika level za Upendo Kilahiro na Miriam Lukindo
Angel Bernard akiwaongoza wenzake kumsifu Mungu wakati wa utolewaji wa tuzo za muziki wa injili Tanzania.

0 comments:
Post a Comment