Social Icons

Saturday, July 16, 2011

VODACOM MISS EXCELLENCE OUT 2011 HUYU HAPA

Vodacom Miss Excellence OUT 2011 Neema Mtitu akipunga mkono mara baada ya kutangazwa mshindi kati ya warembo 10 waliokuwa wakigombea kinyang;anyiro hicho juzi katika viwanja vya Chuo kikuu Huria cha Tanzania.
Vodacom Miss Excellence out 2011 akipunga mkono baada ya kutangazwa mshindi katika shindano lililofanyika katika Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam,kushoto ni mshindi wa pili Weirungu David na mshindi wa tatu Neema Saimoni.
Mshindi wa pili wa Vodacom Miss Excellence 2011 Weirungu David akipokea Hundi yenye thamani ya shilingi milioni 6,030,000 kutoka kwa Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Afrika Kusini katika shindano lililofanyika viwanja vya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe akimpongeza Vodacom Miss Excellence Out 2011 Neema Mtitu kushoto ni mshindi wa pili Weirungu David na mshindi wa tatu Neema Saimoni.
Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 6,030,000 Vodacom Miss Excellence out 2011 Neema Mtitu katika shindano ilililofanyika viwanja vya Chuo Kikuu Huria cha Dar es Salaam juzi.
Washiriki wa shindano la Vodacom Miss Excellence out 2011 waliofanikiwa kuingia katika hatua ya Tano bora wakiwa katika picha ya pamoja.kutoka kushoto ,Weirungu David,Neema Saimoni,Sophia Chacha, Hadija Madege na Neema Mtitu.
picha: fullshangweblogspot.com

0 comments: