Social Icons

Sunday, July 24, 2011

STELLA MBUGE ALAMBA TAJI LA REDD'S MISS KINONDONI 2011

Miss Kinondoni 2011, Stella Mbuge (katikati), akiwa kwenye pozi la pamoja na mshindi namba mbili, Husna Mauld (kushoto), na mshindi wa tatu Khamisa Hassan, muda mfupi baada ya kutwaa taji hilo.
Majaji wa shindano hilo wakichakachua matokea muda mfupi kabla ya kutaja matokeo.
Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper (kushoto), akiwa kwenye pozi na mshindi wa pili wa kinyang'anyiro hicho Husna Mauld, mara baada ya kumkabidhi zawadi yake.
Miss Kinondoni 2011, Stella Mbuge, akipokea zawadi ya tv kutoka kwa wawakirishi wa Star Times, mara baada ya kutangazwa mshindi.
Msanii wa sarakasi akionyesha uwezo wake

Wasanii wa filamu Bongo, Yusuf Mlela (kulia), na Jacqueline Wolper, wakibadilishana jambo ukumbini hapo.
Wasanii wakiigiza miondoko ya Michael Jackson
Miss Tanzania 2007, Richa Adhia, akiwa kwenye pozi na rafiki yake
Msanii kutoka THT, Mataluma, akitumbuiza mahari hapo
Husna akionyesha kipaji chaka wakati wa kumsaka mrembo mwenye kipaji
Baadhi ya watazamaji wakishangaa moja ya shoo zilizokuwa zikitolewa
Mrembo na vazi la Beach
Wasanii kutoka kwenye nyumba ya kukuza viapaji (THT), wakionyesha uwezo wao
Walipagawisha namna hii
Warembo waliyobahatika kuingia kwenye nafasi ya tano bora wakiwa kwenye pozi la pamoja
Warembo walipendeza kama unavyoona mdau
Mrembo akijitambulisha na vazi lake la ubunifu
Mrembo katika pozi tayari kwa kuonyesha vazi la ubunifu
Mambo ya ubunifu
Ishu haikuwa ndogo pande hizo
Washiriki katika vazi la ubunifu
Mambo yalikuwa hivi wadau
Husna Mauld akionenyesha vazi la ubunifu
Vazi la ubunifu lilitawala
Mrembo na vazi hilo
Mrembo aliyetwaa taji la nidhamu kambini Elinarda, akijitambulisha kwa mashabiki Ukumbini hapo.
Mmoja wa washiriki wa kinyang'anyiro hicho akijitambulisha kwa mashabiki
Warembo wakpita jukwaani kuonyesha vazi la ubunifu
Vazi la ubunifu lilitawala namna hii
Mshiriki akinadi vazi lake la ubunifu

MSHIRIKI wa kumsaka mrembo wa miss Kinondoni 2011, Stella Mbuge, usiku wa kuamkia leo ametwaa taji hilo baada ya kuwabwaga washiriki wenzake zaidi ya 13, waliyokuwa wakichuwana ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambapo mshindi huyo alijinyakulia kitita cha zaidi ya dolla 1,000 za Kimarekani na tv nchi 32 kutoka Star Times.
Nafasi ya pili ilinyakuliwa na Husna Mauld, ambaye alilamba kitita cha dolla 800, za kimarekani na mshindi wa tatu, Khamisa Hassan, alilamba dolla 800, za kimarekani, huku akipata na milioni moja ya za Kitanzania na taji la Balozi wa Giraffe Hotel.
Katika mashindano hayo, miss aliyekuwa amevalia namba 6 Fatma Pombe, ndiye aliyenyakuwa taji la miss mwenye kipaji na alipewa zawadi ya dolla 400, za Kimarekani.

0 comments: