Social Icons

Wednesday, July 6, 2011

NAIBU SPIKA AFANYA ZIARA MJINI READING -UK

Frank (kushoto) akiongea jambo Na Mh Naibu Spika Job Ngungai(katikati) akiwa na Mwenyekiti Wa Tanz Uk Dr John Lusingu
Mwenyekiti wa Tanz Uk Dr Lusingu(Kulia), akiwa kwenye mazungumzo na Naibu Spika Mh Job Ndungai aliye katikati, (kushoto), ni mjumbe wa kamati hiyo bwana Frank.

NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndungai , pamoja na shuguli nzito za kuongoza Ujumbe wa Wabunge walioliwakilisha Taifa katika majadiliano ya BAE Uingereza, alitumia fursa ya siku ya mapumziko siku ya Jumapili na kufanya ziara fupi ili kujifahamisha zaidi kuhusu shuguli za Diaspora nchini Uingereza.

Akiwa mgeni wa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Kitaifa, Dr John Lusingu katika makazi yake mjini Reading, Mheshimiwa Ndungai , alipata muda wa kufahamishwa jinsi ambavyo Jumuiya ya WaTanzania(TANZ-UK), ilivyojipanga kushiriki katika mipango mbali mbali ya maendelo ya Taifa, pamoja na kuwatumikia waTanzania waishio nchini humo.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kiTaifa, alimpongeza Mh Ndungai kwa kukubali kuongoza shuguli hiyo ya mashauriano pamoja na changamoto zake.

Dr Lusingu alisisitiza kuwa chaguo la sector ya Elimu kama “mfaidi mlengwa” ni jambo la kuungwa mkono na kila Mtanzania baadala ya kuangalia kila jambo katika mapungufu zaidi ya faida.
Dr Lusingu alimuahidi Mh. Ndungai kuwa, kwa wakati muafaka, Jumuiya itawasiliana na vyombo husika kuweza kuweka rasmi mkakati wa Jumuiya kujishirikisha na shuguli za bunge. Kwa sasa Jumuiya isingependa kuchanganya mambo.

Ajenda kwa sasa ni kuhakikisha kuwa lengo la ujumbe wake linafanikishwa kwanza.
Mh. Ndungai alifurahishwa na mikakati ya Diaspora ambayo aliita ya kizalendo na yenye njozi zinazokubalika.
Mh. Ndungai, pia alifurahishwa zaidi kusikia kuwa Diaspora ni mojawapo ya mafanikio ya serikali ya awamu ya nne.
Mh. Ndungai alikubaliana na kauli ya Dr John Lusingu, kuwa kwa wakati muafaka, bunge kupitia vyombo husika vya serikali litajitahidi kushirikiana na Diaspora katika maeneo mbali mbali ya ujenzi wa Taifa.



0 comments: