Social Icons

Saturday, June 18, 2011

MOTO MKALI WATIKISA DODOMA


Moto mkali uliodumu kwa saa mbili, umetikisa eneo la Dodoma Mjini, huku ukiacha umeteketeza upande wa Hoteli ya Calman na fremu tano zenye maduka na saluni za kike na kiume.

Hoteli ya Calman ambayo ipo Mtaa wa Kondoa, jirani na Makao Makuu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeungua upande wa mgahawa na hakuna kilichookolewa.

Inaelezwa kwamba moto huo ulianza kuwaka saa 9:00 usiku lakini licha ya askari wa kikosi cha zimamoto kuwahi kufika eneo la tukio lakini ilibidi wasubiri mpaka saa 11:00 alfajiri ili kuuzima.
Hoteli hiyo ambayo mmiliki wake ni Haleluya Wilfred, haikuelezwa chanzo cha moto wake ni nini, kwani kila aliyehojiwa alidai hafahamu chochote.

Chanzo chetu kinasema kuwa baada ya moto huo kushika kasi kwenye mgahawa huo, ulihamia kwenye fremu za maduka yanayopakana na hoteli hiyo.mateja20 ilifika eneo la tukio saa 10:18 usiku na kukuta moto ukishika kasi, huku wakazi wengi wa eneo hilo wakiwa nje, wangine wakishangaa, ingawa wapo walioshirikiana na askari wa zima moto kuzima.

Thamani halisi ya mali zilizoharibiwa haijafahamika lakini sehemu ya mgahawa katika hoteli hiyo, yote imeteketea, wakati maduka mawili, saluni mbili za kike na moja ya kiume, vyote vikiwa vimeteketea.
Wamiliki wa maduka hayo, wametajwa kwa majina moja moja kuwa ni Halima, Venose, Frida na Kampuni ya Pagamon.

Baadhi ya watu walibaki kushngaa.

Mama akifarijiwa baada ya duka lake la vipodozi kuteketea lote.

Hawa wakiwa wameshikwa na bumbuwazi, wasijue la kufanya

Askari wa zima moto akiondoa ngazi baada ya kufanikiwa kuzima moto huo.


Bibi akifarijiwa.

0 comments: