Picha ya kwanza juu Mbuyanze akiongea kwa msisitizo wakati akitangaza uzinduzi huo kwa wanahabari kwenye mkutano uliofanyika leo Hoteli ya Hadees jijini. Kulia ni Rais wa bendi hiyo Christian Bella.
Inayofata Rais Msaidizi wa Akudo Impact, Tarcis Masela (kulia) akiwa na mwanamuziki mwenzake wa bendi hiyo, Zagreb Butamu, wakikanusha habari zilizotapakaa kuwa wamehama kwenye bendi hiyo baada ya mikataba yao kumalizika.
BENDI ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’, leo imetangaza kuzindua albamu yake ya pili iitwayo ‘History No Change’. Meneja Masoko wa Bendi hiyo, Patrick Mbuyanze, alisema uzinduzi wa albamu hiyo yenye nyimbo nane utafanyika Julai 2 mwaka huu, Ukumbi wa Vatican City uliopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Rapa wa Akudo Impact, Totoo Zebingwa (katikati) akitangaza kuzindua albamu yake iitwayo ‘Kitu hii haieleweki’ katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam Julai 1 mwaka huu, siku moja kabla ya uzinduzi wa albamu ya bendi yake. Aliokaa nao ni miongoni mwa wadhamini wake katika uzinduzi huo.
Wanahabari wakiwa kazini kuwasikiliza Akudo Impact.
Wanahabari wakiwa kazini kuwasikiliza Akudo Impact.
0 comments:
Post a Comment