Ndugu Zangu,
ABRAKADABRA ni neno lisilo na maana yoyote yenye kueleweka na kuleta mantiki. Mwenye kuongea na kujifanya anafanya vitu vya miujiza na vya kimazingaombwe kimsingi anachofanya ni abrakadabra, hata kama halitamki neno hilo. Ni mambo yasiyo na uthibitisho wa kisayansi na mara nyingi wenye kutenda hudai kuwa ’ wameoteshwa’ na kumhusisha Mungu, hivyo basi, huwezi kuthibitisha kisayansi.
Na Watanzania tunaumwa kweli. Tumekuwa wagonjwa wenye kutafuta chochote kile ili tupate nafuu ya maradhi yetu. Na ’ watalaamu’ wa tiba ya maradhi yetu wanatugombania. Ndio, ni wagonjwa tunaogombaniwa. Si tumemsikia Askofu fulani wa Kanisa la kule Mwenge, tayari amemshambulia ’ Babu’ hadharani. Anatishia kumchukulia ’ wagonjwa’ wake! Askofu nae ni ’ mgonjwa’- maradhi yake ni pesa, hatosheki.
Na si tumemsikia ’ Babu’ wa Loliondo anavyojisifu na kujitangazia unabii? Anasema; “Na kama nilivyokueleza, mimi ni Mchungaji mstaafu lakini pia ni “Nabii” ambaye naweza kuona maono au ndoto na kuzungumza na Mungu mara kwa mara . Na yote ninayoyatekeleza kama unavyoona ni maagizo ya Mwenyezi Mungu.”
“Nimefanya kazi za uchungaji tangu mwaka 1967 katika sehemu kadhaa nchini hadi mwaka 1989 nilipohamishiwa katika eneo hilo. Na nimefanya kazi za uchungaji hapa hadi nilipostaafu mwaka 2002”
‘Nilianza kuota maono na kusikia sauti ya Mungu tangu mwaka 1991 ikinieleza kuwa nibaki kuishi eneo hili; kwani Mungu alikuwa anataka kunipa kazi maalumu ambayo kwa wakati huo sikuifahamu” ( RAIA MWEMA NA: 176)
Sitatafuna maneno bali kuweka bayana, kuwa hayo ya ’ Babu’ wa Loliondo ni abrakadabra. Kwa wajanja neno hili Abrakadabra ni neno la ajabu, neno la miujiza. Kwa kawaida neno hulala, lakini abrakadabra laweza kusimama katika pembe tatu.
Zama hizi, ambapo watu wengi wamekumbwa na hali ya umasikini mkubwa, ujinga na maradhi, kumeibuka manabii wa siku za mwisho. Wenye kunufaika na hofu za wajinga, masikini na wenye maradhi kwa kutumia abrakadabra. Lakini abrakadabra inatumika pia kututoa kwenye kujadili mambo yetu ya msingi.
Manabii hawa wa kujitangaza hufika mahala wakawa na nguvu kiasi cha kuwa na ushawishi mkubwa. Mwandishi Danny Sofe katika kitabu chake; "His Exellency Head Of State" (Mheshimiwa Mkuu wa Nchi) anabainisha hili kwa kumchambua mmoja wa wahusika wakuu katika kitabu hicho. Moses Akaba,
Bwana huyu, Moses Akaba alikuwa Mwalimu na msomi wa uchumi na maarifa ya Biblia. Mwanafunzi mmoja wa shule yake alianguka ghafla na kuzimia. Alipelekwa hospitalini na kudhaniwa kuwa amekufa, mara alizinduka ghafla. Akaelezea kisa chake, kwamba alijikuta akiwa kwenye handaki jembamba na lenye giza. Mwisho wa handaki hilo kulikuwa na mwanga.
Alipoukaribia mwanga alimwona mtu aliyevalia joho jeupe. Mtu huyu alimwambia kuwa Mungu alimtaka arudi tena duniani kwa vile kazi aliyotakiwa kuifanya duniani alikuwa hajaimaliza. Kwamba wazazi wake masikini walimwihitaji.
Kijana huyu aliamini kuwa mtu yule mtakatifu aliyekutana naye kwenye mpaka wa mauti na uhai alikuwa Moses Akaba, mchumi na msomi wa maarifa ya Biblia na ambaye alikuwa mwalimu katika shule ya kijana yule. Baada ya kusikia kauli ya kijana yule, Moses Akaba akajitangaza kuwa nabii, akaanzisha kanisa la Life-After -Life (Maisha Baada ya Maisha.)
Nabii Akaba alikuwa hodari sana wa kulitawala jukwaa na kuzungumza katika hadhara. Akaba alikuwa na mbinu na uwezo mkubwa wa kushawishi. Watu wengi na hasa masikini walijiunga na kanisa lake. Walichanga pesa na vito vyao vya thamani.
Na Watanzania tunazidiwa na WaNigeria tu katika dunia hii katika mambo ya abrakadabra. Na foleni za kwa ' Babu' Loliondo zitapungua mara ile Watanzania watakapoamka kuwa abrakadabra ya ' Babu' ni miyeyusho. Lakini kwa vile bado tunaumwa, basi, tunabadilisha ' hospitali'.
Naam. Hakuna lililo bora kwa mwanadamu kama kuwa na hekima. Kwa mwanadamu, kuelewa jambo hutanguliwa na kutanabahi. Ina maana ya kufikiri kwa umakini na kugundua undani wa mambo. Ni bahati mbaya, kuwa wengi wetu tu wavivu sana wa kutanabahi.
Ndio, tumekuwa ni watu wa kufuata mkumbo wa fikra, hatujipi tabu ya kutanabahi. Jambo hili laweza kuwa na madhara makubwa. Zamani sana alipata kutokea mtabiri wa nyota katika mji mmoja mdogo kule Ulaya.
Huyu alitawatabiria watu wa mji huo , kuwa katika tarehe fulani kungetokea kimbunga kikubwa. Kimbunga hicho kingeangamiza majengo na kuna watu wangepoteza uhai. Salama yao? Ndio, pindi dalili za kuanza kwa kimbunga hicho zingeonekana, basi, wakazi wa mji huo waharakishe kuelekea Kaskazini ya mji huo kuliko na milima.
Jioni moja giza lilianza kuingia katika siku iliyotabiriwa. Ikafika saa tatu za usiku bila kuonekana kwa dalili za kimbunga. Ghafla, bwana mmoja kupitia dirisha lake aliona gari likitoka kwa kasi ya kutimua vumbi kutoka nyumba ya jirani. Bwana yule aliamini kuwa kimbunga hicho sasa kimeingia kwenye mji wao na kwamba jirani yake alikuwa akikimbia na familia yake kuokoa maisha yao.
Bwana yule naye akaamrisha familia yake kuingia ndani ya gari. Naye akaondosha gari lake kwa kasi ya kutimua vumbi kuelekea Kaskazini ya mji. Mwenye nyumba nyingine baada ya kuona gari mbili zikipita kwa kasi nje ya nyumba yake, naye akaamini kimbunga kilichotabiriwa kimewadia. Akabeba familia yake na kutimua vumbi na gari lake. Kuona hivyo, wakazi wa mji huo, mmoja baada ya mwingine, wakaanza kukimbia mji wao kuelekea Kaskazini wakihofia kimbunga. Kijiji kizima kikahama!
Huko walikokimbilia wakaanza kuulizana; Ilikuwaje? Ikabainika, kuwa yule bwana wa kwanza aliyevurumisha gari lake alikuwa amegombana na mkewe, na aliamua kuondoka nyumbani kwake akiendesha gari kwa kasi akiwa na hasira, basi. Na hasira zilipomwisha akajirudia nyumbani kwa mkewe!
Tuna cha kujifunza katika kisa hicho. Si tunaona, kuwa sasa kila mmoja anamzungumzia ’ Babu’ wa Loliondo. Wengi wanafunga safari kwenda Loliondo. Hatutumii muda mwingi kujiuliza; Ya kwa ’ Babu’ Loliondo yalianzaje? Na je, kama ’ Babu’ wa Loliondo ana dawa ya kutibu kansa, kisukari na hata UKIMWI kuna uthibitisho wa Kisayansi?
Na mengine ni rahisi kuyapima hata kwa masikio kujua kama kuna ukweli. Fikiria, maelfu haya ya watu waliopata ’ Kikombe Cha Babu’, kama kungekuwa na watu mia tano tu waliopona, basi, tunashindwaje kuwapata watu ishirini miongoni mwao wa kututhibitishia kisayansi, kuwa walikuwa na maradhi hayo sugu kabla na sasa wamepimwa na hawana tena.
Ni mtazamo wangu, kuwa hii ya kwa ’ Babu’ Loliondo ni Abrakadabra nyingine. Serikali ilikuwa haina sababu ya kubabaika katika kulitolea msimamo hili la Loliondo. Msimamo wa awali ulikuwa sahihi kabisa; kusimamisha zoezi la utoaji wa tiba hiyo mpaka Serikali itakapojiridhisha juu ya dawa hiyo kupitia uchunguzi wa kisayansi.
Ndio, Serikali ilipaswa kuueleza umma, kuwa kwa sasa dawa hiyo haitambuliki kisayansi, haijafanyiwa uchunguzi, inahitaji kufanyiwa uchunguzi ili kuhakikisha, sio tu kama inatibu, bali kama ina madhara kwa mwanadamu. Hilo ni jukumu la Serikali katika kulinda usalama wa watu wake. Na huko hakutakuwa kuingilia masuala ya imani za watu.
Maggid

0 comments:
Post a Comment