Social Icons

Tuesday, March 15, 2011

WAZIRI MKUU AWATUNUKU VYETI WATUMISHI WA OFISI YAKE

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi Katibu Mkuu wa zamani katika Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Maimuna Tarishi katika hafla ya kuwaaga watumishi wa Ofisi yake waliohamishwa kwenda Wizara nyingine na wale waliostaafu. Hafla hiyo ilifanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Machi 13, 2011. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Mbunge wa Hanang, Dk. Mary Nagu.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi Cheti cha Utumishi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Ignas Kaduma katika hafla ya kuwaaga watumishi wa Ofisi yake waliohamishwa kwenda Wizara nyingine na wale waliostaafu. Hafla hiyo ilifanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Machi 13, 2011. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Mbunge wa Hanang, Dk. Mary Nagu.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

0 comments: