Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge),William Lukuvi, akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa tamko la Serikali kuhusu Kamati iliyoundwa na Serikali kwa ajili ya kwenda Loliondo kumsaidia Mchungaji Mwasapila kuendelea na kutoa huduma kwa wananchi wanaofika nyumbani kwake kwa ajili ya kunywa dawa.
---
Alisema kuwa Serikali haijazuia tiba hiyo kutoka kwa Mchungaji huyo, na wala haina mpango wa kuzuia ila kutokana na uwingi wa watu na magari yaliyokwama katika Kijiji hicho kuna kila sababu ya Serikali kuingila kati ili kuweza kunusuru maisha ya wananchi hao kabla ya kutokea maafa makubwa.
Aidha alisema kuwa Serikali kupitia Kamati yake iliyoundwa kwa kushirikiana na Serikali ya Kijiji hicho pamoja na Mkuu wa Mkoa huo, wamejipanga kuanza kuzuia magari yote yanayoingia kijiji hicho ili kupunguza msongamano uliopo na badala yake waruhusu magari kutoka tu hadi hapo yatakapopungua na kujipanga kuanza kutoa huduma hiyo kwa utaratibu ili kuepuka msongamano ulioishatokea.
Lukuvi, aliwashauri Wananchi waliokwishafanikiwa kupata huduma hiyo kwenda katika vituo vya afya na kupima afya zao baada ya siku 14 tangua walipokunywa dawa hiyo ili kuweza kuona kama kunamabadiliko ama la, wakati Serikali kupitia Kamati yake ikiendelea na kuifanyia kazi dawa hiyo kuweza kubaini ubora wake na Dozi yake kwa ujumla, ili iweze kuwa katika kiwango cha TBS.
Mbali na Kamati hiyo pia Serikali imejipanga kupeleka magari ya kubebea wagonjwa eneo hilo ili kuweza kutoa huduma ya kuwawaisha waliozidiwa katika mahospitali, pamoja na kuandaa huduma za afya kama vyoo na mahema ya kupumzikia wananchi wanaokuwa wakisubiri kupata huduma.
Picha na Habari na Mdau Sufiani Mafoto

0 comments:
Post a Comment