Mtangazaji wa kituo cha ITV na Redio One, ambaye ni mshambuliaji wa TASWA FC, Maulid Kitenge (kushoto), akimtoka beki wa Polisi Jamii, msanii na muongozaji wa filamu, William Mtitu.
MAOFISA wa Jeshi la Polisi nchini wakiongozwa na Kamishna Mkuu wake, Said Mwema, jana walizindua michuano ya kombe la Kamanda Kova, katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Michuano hiyo ilizinduliwa kwa mechi kati ya timu ya waandishi wa habari (TASWA FC) na Polisi Jamii ambapo TASWA walifungwa mabao 3-1.
Kamanda Kova akikumbatia mpira baada ya kudaka shuti la Maulid Kitenge.
Mshambuliaji wa Polisi Polisi Jamii, Lukas Mhuvile almaarufu kama Joti (kushoto) wa kundi la Orijino Komedi akimtoka beki wa TASWA FC.
Mechi hiyo ilikuwa ikitangazwa ‘live’ uwanjani hapo na msanii wa kundi la Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’
Mchezaji wa Polisi Jamii, Jacob Steven ‘JB,’ akitoka nje ya uwanja baada ya kutolewa.
Msanii wa filamu, Dokii (kushoto) akitaniana na Joti (kulia) uwanjani hapo.
0 comments:
Post a Comment