Mtu huyo akiwa amelala chini katika kituo cha Bamaga.
MTU mmoja (kijana) ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja alitupwa kutoka kwenye gari moja katika kituo cha mafuta cha Bamaga kilicho maeneo ya Mwenge, jijini Dar es Salaam, majira ya saa nane na nusu usiku.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa gari moja dogo lilifika eneo hilo kisha wakateremka vijana wanne, wakafungua buti la gari hilo na kumchomoa kijana huyo na kumtelekeza hapo kabla ya kuondoka kwa mwendo wa kasi.
Katika kufuatilia, mtandao huu ulipata habari za kipolisi ambazo zimesema kijana huyo yu hai akiwa amelazwa hospitali ya Mwananyamala jijini, japokuwa hali yake ni mbaya. Vilevile, kisa cha tukio hilo hadi tunakwenda mtamboni kilikuwa hakijajulikana.
Polisi wa kituo cha Oster Bay wakimbeba kijana huyo kumwingiza katika gari.
0 comments:
Post a Comment