Rais Jakaya Kikwete ( wa pili kulia) akimshukuru mshauri wa Mambo ya Nje wa China, Ji Pedin baada ya kusaini mikataba ya makubaliano ambapo Serikali ya China imekubali kuisaidia Tanzania katika masuala ya maendeleo ya elimu na ujenzi wa mkongo wa mawasiliano Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu Dar es Salaam jana. Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Khamis Dihenga (kulia) akibadilishana hati za makubaliano na Katibu Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wa China, Meng Tu baada ya kutiliana saini mkataba ambapo Serikali ya China imekubali kuisaidia Tanzania katika masuala ya maendeleo ya elimu kwa kujenga shule za matumaini. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam jana.
Picha na Richard Mwaikenda
Picha na Richard Mwaikenda
0 comments:
Post a Comment