Nyoshi El Sadat na Queen Suzy.
RAIS wa bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Nyoshi El Sadat ‘Sauti ya Simba’, leo “amevamia” ofisi za Global Publishers na kumtambulisha, Suzanne Chubwa ‘Queen Suzy’ mnenguaji aliyetokea bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’.
Akizungumza na wanahabari, Nyoshi amesema alifurahia kurejea kwa mnenguaji huyo katika bendi hiyo baada ya kuwaacha takribani miaka miwili iliyopita.
“Nimekuja kuwatambulisha kuwa Suzzy amerudi nyumbani na ameshaanza kazi hivyo mtambue kuwa ni mali ya Ngwasuma,” alisema Nyoshi kwa majigambo na furaha.
Aliongeza pia kwamba bendi yake iko mbioni kuwarudisha wanenguaji wote waliowahi kufanya kazi na bendi hiyo kwani anathamini sana mchango wao ndani ya bendi hiyo.
…Akibadilishana mawazo na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Richard Manyota (kushoto).
…Akiwa na Queen Suzy kwenye ofisi ya Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto).
Mhariri kiongozi wa magazeti ya Championi, Saleh Ally (kulia) akiwa na wanamuziki hao.
0 comments:
Post a Comment