Adelqueen (katikati) akizungumza na wanahabari. Kulia ni mshindi wa pili wa taji hilo, Happywhitney Andrew na kushoto ni mshindi wa tatu, Maria Rabii.
MREMBO aliyetwaa taji la Miss Utalii Taifa, Machi 5 mwaka huu Bagamoyo mkoani Pwani, Adelqueen Njozi, leo amezungumza na wanahabari katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam na kueleza baadhi ya mambo atakayoanza nayo wakati akifanya shughuli za kijamii na kuitangaza sekta ya utalii hapa nchini.
Adelqueen aliyataja baadhi ya mambo kuwa ni kuielimisha jamii juu ya utalii, kupiga vita utamaduni wa tohara kwa wanawake na uwindaji, uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira.
Miss Utalii akiwa amepozi kwenye kiti.
PICHA: RICHARD BUKOS / GPL
0 comments:
Post a Comment