Meya wa Halmashauri ya Ilala, Jerry Slaa (kushoto), akisikiliza hotuba ya Meya wa Halmashauri ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (katikati), kulia ni Asha Baraka.
WATANZANIA waishio Uingereza Ijumaa iliyopita walishirikiana na bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani’ kufanikisha harambe ya kuwachangia waathirika wa milipuko ya mabomu iliyotokea hivi karibuni Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Twanga Pepeta ilifanya onyesho maalum Machi 4 mwaka huu katika ukumbi wa Zhong Hua Garden uliopo Mikocheni, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es Salaam na kupata kiasi cha sh. milioni mbili zitakazowakilishwa kwa waathirika hao.
Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka, alisema katika harambe hiyo pia walichangiwa kiasi cha sh. milioni moja (1,000,000/=) na kundi la ‘Saidia Gongo la Mboto’ toka Uingereza.
Miongoni mwa vitu vilivyochangwa na kundi hilo ni pamoja na chakula, nguo na vitabu ambavyo bado viko kwenye makontena vikiwa njiani kutoka Uingereza ambapo vitapokea siku chache zijazo.
Asha Baraka alisema shughuli hiyo ya ukusanyaji wa michango hiyo ya Uingereza iliandaliwa na Miss Jestina, Shilla Frisch kutoka miss jestinageorge blog pamoja na Frank Eyembe na Baraka Baraka Urban, Chisumo kutoka Locus Impex Shipping Co.
Asha Baraka akitoa mchango uliopatikana kwenye hafla hiyo.
0 comments:
Post a Comment