Mwenyekiti wa Baraza la walaji/watumiaji kutoka SUMATRA Bw. Guliadi Ngewe akitoa ufafanuzi kwa waadishi wa habari juu ya kupanda kwa viwango vya nauli za usafiri(daladala) katika jijini la Dar es salaam na mikoa mingine.Amefafanua kuwa ongezeko hilo linatokana na kupanda kwa gharama za mafuta duniani na ongezeko la vitendo vya uharamia katika bahari ya Hindi huku akibainisha kuwa jiji la Dar es salaam lina waendesha huduma za usafirishaji 3500 na tayari mapendekezo ya kuwa na makampuni ya uendeshaji wa shughuli za usafirishaji yameshawasilishwa serikalini.
Mwenyekiti wa Jukwaa la mabaraza ya watumiaji/walaji Tanzania (TFC) Eng.Prof. Jamidu Katima (kushoto) akizungumza na wadau wa Jukwaa la mlaji/mtumiaji pamoja na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mlaji Duniani 2011 itakayoongozwa na kauli mbiu “ Huduma za Kifedha ni Stahiki ya watumiaji” yenye lengo la kusisitiza uwazi, taarifa sahihi, haki na huduma bora za kifedha kwa mtumiaji leo jijini Dar es salaam. Kulia ni mwenyekiti wa Baraza la watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na TCRA (TCRA –CCC) Bi. Hawa Ng’humbi.

0 comments:
Post a Comment