Social Icons

Monday, March 14, 2011

KISUMA BAA YASHINDA MPAMBANO WA NYAMA CHOMA

Wachoma nyama wa Kisuma Bar wakiwa mzigoni.

BAA ya Kisuma iliyoko Tandika Mwembe-Yanga jijini Dar es Salaam, jana iliibuka kwa mara ya pili mfululizo na kushinda shindano la “Safari Lager Nyama Choma” lililofikia tamati jana katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. Baa hiyo ambayo imeshinda mpambano wa baa yenye kuchoma nyama bora zaidi, ilikabidhiwa kitita cha Sh. 1,000,000 (milioni moja) na kupewa cheti maalumu kutoka katika Kampuni ya Bia nchini (TBL).



Baadhi ya watu wakichagua nyama zilizo tayari kuliwa.


Wafanyakazi wa baa hiyo wakiwa wamembeba mwenzao, Jerome Kavishe, kwenda kupokea zawadi yake.


…Akiwa na mbunge wa Kinondoni, Mheshimiwa Idd Azzan, baada ya kukabidhiwa zawadi yake.


…Akihesabu kitita chake.

0 comments: