Social Icons

Sunday, March 13, 2011

KAMATI YA BUNGE YA MASHIRIKA YA UMMA YAMUANIKA NGELEJA

Mbunge wa jimbo la Ileje Mbeya ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya bunge hesabu ya mashirika ya umma Mhe.Aliko Kibona akionyesha sehemu ya vitendea kazi vilivyokaa bila kutumika katika mgodi ya kiwira Mbeya
Makamu mwenyekiti wa kamati ya bunge hesabu za mashirika ya umma Mhe.Deo Filikunjombe akitazama mashine zilizosimama bila kutumika katika mgodi wa Kiwira Mbeya
Mwenyekiti wa kamati ya bunge hesabu za mashirika ya umma Mhe.Zitto kabwe akiwatuliza wafanyakazi wa mgodi wa Kiwira ,wasihujumu mgodi huo pamoja na serikali kuchelewa kuwalipa mishahara yao
Mbunge wa viti maalum Tanga Mhe.Amina Mwidau na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Deo Filikunjombe wakitazama kibelenge mgodi wa Kiwira
Wajumbe wote wa kamati ya bunge hesabu wa mashirika ya umma wakiwa na wawekezaji wapya wa mgodi wa Kiwira na wale wa zamani.
---
SAKATA la madai ya wafanyakazi wa mgodi wa makaa ya mawe wa kiwira Mkoani Mbeya limechukua sura mpya baada ya kamati Bunge ya mahesabu ya mashirika ya umma kubaini serikali ilitumia siasa kuwadanya wafanyakazi hao.

Hayo yalibainika jana Mjini hapa mara baada ya kamati hiyo chini ya mwenyekiti wake Zitto Kabwe, kuibua hoja na kutaka ufafanuzi juu ya kauli ya waziri kuhusu serikali kuchukua kiwanda hicho na kubainika hakuna taratibu za kisheria zilizofanyika katika kuchukua kiwanda hicho.

Mara baada ya kuibuliwa hoja hiyo na mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara (CCM) Kangi Lugora, aliyetaka kujua ukweli kuhusu sakata hilo hali iliyopelekea wafanyakazi kuendelea kudaia madai yao ya fedha ikiwamo nauli mishahara ya mwezi Februari mwaka huu.

“Hapa katika hili Mwenyekirti mbona hatuelewi na kuna nini na nakubalina na nawe mwenyekiti kwa hili ilitumika siasa kuliko halisi kwa nini Waziri alifanya hivyo na lazima kupitia kamati yetu atupe majibu ya kina” alisema Mangungu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe, alisema pamoja na juhudi zilizofanyika llaini bado hakuna ushahidi wa ki8sheria ulifanyika katika kuhakikisha mgodi huo kuonyesha kurudi serikalini.

Alisema toka serikali itoe tamko la kulipa malimbilikizo ya madeni ya watumishi wa kiwanda hicho lakini bado mwekezaji aliyeingia ubia na serikali kampuni ya Tan Power Resourses, kupitia kampuni yake ya KCPL, inaonyeswha kuwa bado ni miliki halali wa mgodi huo.

“Hapa hakikisha Waziri Ngeleja, aliwadanganya Wafanyakazi, hakuna utaratibu wowote wa kisheria unaonyesha mgodi kurudi serikalini, ndio maana sasa kuna mchakato wa kuhakikisha NSSF wanapatiwa kiwanda hiki ili wakiendeshe kwa taratibu nzuri ili kuweza kuzalisha na kuzalisha umeme mgodini na hata kuuza kwa Tanesco” alisema Zitto.

Awali akitoa taarifa kwa kamati hiyo Kaimu Meneja wa kiwanda hicho Aswile Mapamba, alisema kutokana na utata ulijitokeza kati ya kauli ya Waziri Ngeleja kuhusu serikali Mgodi huo hadi sasa haileweki nani hasa mmiliki halali wa kiwanda hicho kutokana na kusimamisha uzalishaji na wataalamu wa kada mbalimbali katika mgodi huo kukimbia kutokana na kukosekana na kutolipwa mishahara kwa uhakika.

“Leo tupo hapa lakini hakuna uzalishaji unaondelea kiwandani na waliobaki ni wazee huku kundi la wataalamu wakikimbia, sasa tunaomba kamati yako Mhe. Zitto itupe ufafanuzi wa kweli hali hii hadi lini “ alisema Mapamba.

Hata hivyo alisema tangu kiwanda hiccho kilipoanza kufanya kazi mwaka 2001, walikuwa wakizalisha umeme wa megawati nne huku Tanesco wakliuziwa megawati 3 na kuweza kulipwa kwa wakati tofauti na hivi sasa ambapo hakuna uzalishaji wa aina yoyote unaoendelea kiwandani hapo.

Alisema mkaa wa huo wa mawe zaiodi ya tani 34 milioni kama ungeweza kutumiwa vizuri Tanzania ingenufaika na umeme huo kwa kuzalisha zaidi ya megawati 30 ambzo zingesaidia kupunguza makali ya mgao wa umeme kwa wananchi na kuimarika kwa sekta ya viwanda vikubwa na vidogo.

Meneja huyo alisema toka mwaka 2009 hadi sasa hakuna taarifa ya mdhiti na mkaguzi wa hesabu wa serikali iliyorudishwa ambapo walilazimika kuandika barua zsaidia ya mara tatu ili kuomba taarifa hiyo.

Mwaka 2009, Waziri wa nishati na madini Wiliam Ngeleja, alifika kiwandani hapo na kutamka juu ya serikali kuchukua kiwanda hicho na hadi sasa hakuna juhudi zilizofanyika katika kuhakikisha kiwanda hicho kinarudi serikalini.



Habari /Picha na Mdau Francis Godwin

0 comments: