KATIKA hali iliyoshangaza wengi nikiwemo mimi jana ndani ukumbi wa Mango garden, ilikuwa shamra shamra kama bendi hiyo imepata mwanamziki mpya, lakini ukweli ni kuwa bendi hiyo imepoteza mwanamziki rapa Paul John (Fagason) masaa kama 72 yaliyopita kabla ya onesho hilo la jana jumamosi zilitapakaa habari kuwa Fagason, Rogate Hega, Gody Kanuti, wanenguaji Super nyamwela na mwanadada Otilia bendi ya Ally Choki Extra Bongo. Hatimaye zilithibitika kuwa kweli. walikuwa wametwaliwa na bendi hiyo.
Majira kama ya saa nane na nusu usiku hivi Luiza Mbutu akatangaza kuna kitu anataka kuwaonesha wapenzi wa Twanga waliokuwa wamefurika na ulipofikia muda akamwita Gody Kanuti jukwaani ambaye alikiri kupewa sh milioni sita (6,000,000) ili aihame Bendi hiyo na ajiunge na Extra Bongo lakini alisisitiza kuwa hataki kuhama Twanga na akazitoa pesa hizo pale jukwaani ambapo baadaye alikabidhiwa Asha Baraka. Pia Kanuti ambaye ndiye alipiga gitaa la solo katika wimbo Mwana Dar es Salaam alipewa gitaana na akachombeza kidogo jambo ambalo liliwakuna sana mashabiki wa bendi hiyo ukumbini humo. Kana kwamba hiyo haikutosha Diof naye kaja na Rapu mpya ya Kamata mwizi, ukweli ni kuwa Msafiri Diof kila inaposemekana kwmba kaisha kimuziki yeye huibuka na kitu kipya kama alivothitisha tena jana. Rapu yake hiyo ilipokelewa vizuri na mashabiki kwani kwa uchache Diof labda aliondoka na kama laki mbili hivi za kutunzwa tu. Katika hatua nyingine alipanda jukwaani Kocha wa dunia na kupagawisha mashabiki kiasi kwamba wakaanza kupiga mayowe kwa Luiza Mbutu kwamba achukuliwe Twanga Pepeta. Alimradi tuliokuwemo mle Mango. Garden jana tulipata raha za kutosha. Luiza Mbutu aliahidi kulipeleka ombi la washabiki kwa uongozi likajadiliwe na katika hali isiyokuwa ya kawaida jana mziki ulizimwa saa saa 9.45 za usiku badala ya saa iliyozoeleka saa 9 kamili.
Hamis Kayumbu 'Amigolas' kushoto akiimba pembeni ni Janeth Isinika mwimbaji wa kike katika bendi hiyo.
0 comments:
Post a Comment