KATIKA kuonyesha jitihada za kuwasaidia vijana wanaojaribu kujikwamua kimaisha na hasa wale wanaoonyesha kufaiti katika kutafuta maisha, Mbunge huyo aliweza kutoa ahadi ya kuwasaidia wanamuziki wa bendi mpya ya Mapacha Watatu, Khalid Chokoraa, Kalala Junior na Jose Mara, walioanzisha bendi hiyo siku za hivi karibuni na wawili kati yao kuamua kuachana na habari ya kuajiriwa katika bendi na badala yake wakaamua kujiajiri kwa kufanya kweli na kuwekeza zaidi katika bendi yao ya Mapacha Watatu.
Idd Azan, alitoa ahadi ya kuwasaidia vijana hao kwa kuwasaidia kurekodi nyimbo zaidi ya tano kwa muda wowote watakapokuwa tayari kufanya hivyo.
Mbali na Idd Azan naye mkurugenzi wa Sofia Records, Mussa Kisoki (kulia) alitoa ofa kwa vijana hao ya kurekodi wimbo mmoja na video yake bure katika Studio yake iliyopo maeneo ya Koma Koma Mwananyamala. Ahadi hizi zilitolewa na vigogo hao baada ya kufurahia kazi nzuri iliyotolewa na vijana hao jukwaani walipoonyesha umahiri wao wa kuimba na kucheza kwa bidii na kuwapagawisha mashabiki lukuki waliofurika ukumbini humo kushuhudia uzinduzi huo wa Filamu ya Shoga.
0 comments:
Post a Comment