Jana Uongozi wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta, Sugu Kisima Cha Burudani' Ulifanya hitima kwa ajili ya kumrehemu Meneja na Mpiga Drums wake, Marehemu Abou Semhando aliyefariki dunia Ijumaa iliyopita eneo la Tangibovu Mbezi, jijini Dar es Salaam. Hitma hiyo ilifanyikia Makao Makuu ya bendi hiyo, yaliyopo Kinondoni Vijana jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na baadhi ya wakazi wa maeneo hayo na wapenzi wa bendi hiyo. PICHANI ni baadhi ya wageni waliohudhuria katika shughuli hiyo wakipata chakula cha mchana.
Waigizaji maarufu wa filamu nchini Vicent Kigosi ‘Ray’ (kushoto), akipata msosi na Steven Kanumba ‘Kanumba the Great’ katika shughuli hiyo.
Mbunge wa Kinondoni, Mh. Iddi Azzan (katikati), akijumuika na raia kupata sadaka.
Omari Baraka, mmoja wa viongozi wa Twanga akipata sadaka.
Hassan Mketema ‘Hassan Miundo mbinu’, akikusanya vyombo mara baada ya zoezi la msosi kumalizika.
Mkurugenzi wa Bendi hiyo Asha Baraka (mwenye chupa ya maji) akiongea jambo na baadhi ya wageni waliohudhuria katika shughuli hiyo.
0 comments:
Post a Comment