MAWAKILI wapatao 350 leo wametunukiwa vyeti vya kuwakubali na kuwasajili katika sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee Hall jijini Dar es Salaam, miongoni mwa mawakili hao na mke wa mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani ametunukiwa cheti hicho.
Mgeni rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Jaji Mkuu Augustino Ramadhani.
Jaji mkuu Augustino Ramadhani naye akihutubia katika sherehe hiyo (leo Ijumaa).
Jaji mkuu akisikiliza maelezo kutoka kwa mshehereshaji (Mc) wa shughuli hiyo baada ya kumaliza kuhutubia.
Mheshimiwa Jaji Mkuu akielekea kupiga picha ya pamoja.
baadhi ya mawakili wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu.
Mtoto wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, Ridhiwani Kikwete (kushoto) akibadilishana mawazo na rafiki yake. Ridhiwani alifika hapo kwa ajili ya kushuhudia mkewe akikabidhi cheti chake.
Mke wa Jaji aliyetambulishwa kwa jina la mama Ramadhani akienda mbele kupokea zawadi aliyoandaliwa na waandaaji wa sherehe hiyo.
Mke wa Ridhiwani Kikwete akiwa katika pozi baada ya kukabidhiwa cheti chake.
Ridhiwani Kikwete na mkewe wakiondoka maeneo hayo.
0 comments:
Post a Comment