Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, leo amemuapisha aliyekuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Chande Mohamed Othman kuwa Jaji Mkuu mpya baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, Jaji Augustino Ramadhani, kumaliza muda wake. Jaji Mkuu huyo aliapishwa katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam asubuhi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwa wemo Makamu wa Rais Dk. Ghalib Bilal na Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Pichani ni DK Jakaya akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Chande, Jaji Mkuu aliyemaliza muda wake Agostino Ramadhani (kulia) na Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta
Jaji Chande akila kiapo mbele ya Rais JK huku Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo (kati) akishuhudia
Rais JK akiwa katika picha ya pamoja na majaji wa Mahakama Kuu nchini
Rais akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Chande mara baada ya kumuapisha
viongozi wakielekea kwenye eneo la tukio kabla ya kuanza kwa zoezi la uapishaji
Rais JK akibadilishana mawazo na viongozi wake Mhe. Spika Anna Makinda (wa kwanza kulia), Waziri Mkuu Mhe. Pinda na Makamu wa Rais, Dk Ghalib Bilal.
0 comments:
Post a Comment