Banana Zorro (kushoto) akitumbuiza na baba yake katika onyesho hilo.
Wakati imebakia wiki moja ili uchaguzi mkuu ufanyike nchini, katika viwanja vya Biafra, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, jana kulifanyika tamasha la vijana lililojumuisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya likiwa na lengo la kuuombea uchaguzi huo ufanyikwa kwa haki na amani. Umati mkubwa wa wananchi ulihudhuria tukio hilo lililoanza mchana na kuendelea hadi jioni.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Rashid Marwilo ‘Chidi Benz’, akikamua katika onyesho hilo.
Banana Zorro (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baba yake mzazi, Zahir Ally Zorro.
Farid Kubanda ‘Fid Q’ (kulia) akiteta jambo na Mwana FA.
Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ (kushoto), Hadija Shabani ‘Keisha’ na Fid Q wakiwa katika picha ya pamoja.
Karama Masudi ‘Kala Pina’ akikamua katika onyesho hilo.
Mmoja wa walinzi wa tamasha hilo akiteremka jukwaani baada ya kumtangaza mtoto ambaye alipoteana na ndugu zake uwanjani hapo.
0 comments:
Post a Comment