Social Icons

Monday, October 25, 2010

SIMBA ILIVYOWAPIGISHA KWATA 'WAJEDA'

Beki wa Simba, Juma Jabu (kulia), akiunasua mpira kutoka kwa mshambuliaji wa JKT Ruvu, Hussein Bunu.
TIMU ya Simba, jana iliichakaza timu ya maafande wa JKT Ruvu, kwa mabao 2-1, katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mabao ya Simba yalipachikwa kipindi cha kwanza na Rashid Gumbo, ambapo dakika moja kabla ya mapumziko, Emmanuel Okwi, alipachika bao la pili. Maafande hao walipata bao la kufutia machozi dakika ya 80 lililopachikwa na Hussein Bunu.


Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (mbele), akiwatoka mabeki wa JKT.


Kipa wa JKT, Shaibu Issa (wa pili kushoto), akiruka hewani kudaka moja ya mashuti yaliyoelekezwa golini kwake.


Wachezaji wa Simba wakishangilia goli la kwanza.


Shabiki ambaye hakujulikana jina lake (wa pili kulia) akionekana kutoelewana na askari wa kutuliza ghasia (FFU) baada ya kuingia uwanjani.


Wachezaji wa Simba wakicheza kiduku baada ya kushinda bao la pili.


Mashabiki wa Simba wakishangilia baada ya mpira kumalizika.


0 comments: