Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Tanzania NEC Bw. Rajab Kiravu akizungumza mbele ya waangalizi wa kimataifa wa Uchaguzi Mkuu ujao kutoka mataifa na Jumuiya mbalimbali katika kituo cha kutangazia matokeo ya uchaguzi kilichopo katika Hoteli ya Paradise City, jijini Dar es salaam leo.Wengine katika picha ni viongozi mbalimbali wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Tume ya Uchaguzi imekutana na wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa vyama vya siasa, Msajili wa vyama vya siasa, Wawakilishi wa vyombo vya Usalama na waangalizi wa kimataifa kutoka SADC, Jumuiya ya Ulaya, Jumuiya ya Afrika Mashariki, Canada na mataifa mengine kadhaa ya Ulaya wakiwa tayari kwa kazi iliyowaleta ya kuangalia mwenendo mzima wa Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo Oktoba 31 mwaka huu.
Waangalizi kutoka SADC.
Waangalizi kutoka Jumuiya ya Ulaya.
0 comments:
Post a Comment