Social Icons

Saturday, September 11, 2010

UZINDUZI WA FM CADEMIA FULL SHANGWE!!!


Mkurugenzi mtendaji wa Heineken Beer Benedicta Rugemalila (kushoto) akiwashukulu mashabiki wote mara baada ya kuizindua albama ya sita ya FM Academia Vuta Nikuvute Mathematics 'Mayemba' kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa kuamkia leo ambapo alishirikiana na mkurugenzi masoko wa Kampuni ya Zain Tanzania, Kelvin Twisa wa pili kutoka kulia na anayemfuata ni Felician Mutta, wa kwanza kulia ni 'MC' wa shughuli hiyo Beny Kinyaiya ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa Kinyaiya Pub, iliyopo Kinondoni nyuma ya ukumbi wa Mango Garden.
'Prez Daa' wa Bendi ya FM Academia Nyoshi El Sadaat, wa (pili kushoto) akiongoza jopo la wanenguaji wa kiume wa bendi hiyo mara baada ya kupanda jukwaani tayali kwa uzinduzi wa Albam hiyo ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee.
Shughuli ilikua namna hii baaanaa!!!!.
Wanenguaji wa FM Academia 'Wazee wa Pamba' wakionyesha manjonjo yao jukwaani.
Nameless akiwa amepiga magoti, huku akiigiza kumuimbia wimbo wa Nasisinzia Nikikuwaza, mmoja wa mashabiki waliyekuwepo katika shughuli hiyo, mapema usiku wa kuamkia leo.
Mwanamuziki kutoka nchini Kenya, David Mathenge 'Nameless' akiomba kucheza na mmoja wa mashabiki waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.
Boss wa zamani wa bendi hiyo (kushoto) akitamburishwa na Martin Kasyanju (katikati) kwa Mkurugenzi Masoko wa Zain Kelvini Twissa.
Baadhi ya wageni waarikwa, wakifuatilia uzinduzi huo, uliofanyika ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa kuamkia leo.
Boss wa FM Academia, Martin Kasyanju (kulia) akibadilishana mawazo na mmiliki wa zamani wa bendi hiyo, Felician Mutta na mrs wake (mwisho) ni 'MD' wa Heineken Beer Madame Benedicta Rugemalila katika uzinduzi huo.

Timu nzima ya waimbaji wa FM Academia ikiajibika stejini.

Hapa walizindua ka' beer kapya baana


Nameless ...Bongo freeeshii....


Mwanamuziki mwaarikwa kutoka nchini Kenya, Nameless akicheza na shabiki wakati akisindikiza uzinduzi huo.

Mnenguaji wa FM Academia, Aliyah akiwasalimia mashabiki.

Mc wa shughuli hiyo, Benny Kinyaiya akiwa katika pozi mara baada ya uzinduzi.








0 comments: