Social Icons

Monday, September 27, 2010

PATA HABARI NA MATUKIO TOFAUTI, YALIYOJILI KITAANI!!!

Baadhi wa wanafunzi wakiwa nje ya jingo hilo.
KUNDI la wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kujiunga na vyuo mbalimbali vya serikali na kupata alama za juu leo wamefurika nje ya Jengo la Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) lililopo Mikocheni jijini Dar es Salaam wakipinga uamuzi wa wenzao waliopata alama ndogo kupatiwa nafasi za kujiunga na vyuo vya serikali na wao kukosa nafasi na kudai uamuzi huo ni wa kuwaonea.


Askari wa jengo hilo akiinyoosha mkono kuwataka wanafunzi hao kukaa mbali na eneo hilo, amri yaliyokataa kuitii.


Muuza “lamba-lamba” (ice cream) akiwa kwenye mkusanyiko huo kukata kiu ya ‘madenti’ hao.


Mkali wa miondoko ya Bongo Fleva, Juma Nature (Sir Nature), akipagawisha mashabiki waliohuduria onyesho la “Vuta-Nikuvute” lililofanyika usiku wa kuamkia leo Ukumbi wa Hoteli ya Travertine jijini Dar es Salaam.


Nature akiwa kazini.


…Akiwa amebebwa na mashabiki.


Mkongwe wa muziki wa mwambao, Shakira Said, naye alionyesha ufundi wake katika onyesho hilo.


Mashabiki wakichizika kwa raha zao.

0 comments: