Social Icons

Tuesday, April 26, 2011

BONGO MOVIE WASHINDWA KUTETEA JINA LAO KWENYE BONANZA LA PASAKA TABATA

Mwandaaji wa Bonanza hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Paris Pub, John Mange (kulia), akikabidhi jezi kwa kapteni wa timu ya Long Room, kwenye hafla fupi ya utoaji zawadi hizo, iliyofanyikwe kkatika eneo la Paris Pub.
Bendi ya Extra Bongo, Wazee wa mjini Mipango, wakitumbuiza kwenye Bonanza hilo.
Mmoja wa Wanenguaji wa bendi hiyo akionyesha uwezo wake.
JB, akidokezwa na viongozi wake namna atakavyofanya mara baada ya kuvaa jezi tayali kwa kabumbu.
Beny Kinyaiya, akipasha misuli na JB
JB, akipasha msuli muda mfupi kabla ya mechi yao kuanza.
Baadhi ya mashabiki waliofulika, Viwanjani hapo wakifualia mechi hizo kwa makini.
Dokta Cheni, akisepa mdogo mdogo, mara baada ya timu yao kufungwa.
Papa B2C, akikabizi zawadi kwa washindi wa pili.
Papa B2C, akiongea jambo kwenye hafla fupi ya kukabidhi zawadi hizo, iliyofanyika eneo la Paris Pub Tabata.
Mkurugenzi wa Paris Pub, John Mange, akiangalia zawadi za washindi wake.
Tinno (kulia), akitembea kwa unyonge muda mfupi baada ya mechi hiyo kumalizika
Muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Ruth Suka 'Mainda,' akiangalia kitu kwenye pensi ya mmoja wa wachezaji hao.
Baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wakionekana wenye hudhuni mara baada ya timu yao kufungwa magoli mawili kwa bila

Wachezaji wa timu ya Bongo Movie wakipeana mawaidha muda mfupi baada ya mapumziko.
JB, akichachawa uwanjani hapo.

TIMU ya mpira wa miguu inayoundwa na baadhi ya mastaa kutoka ndani ya Tasinia ya Filamu Bongo, jana jumatatu ya Pasaka, walikuwa wamearikwa kwenye Bonanza la Paska, lililokuwa limeandaliwa na Mkurugenzi wa Paris Pub Bwana John Mange, katika Viwanja vya Shule ya Msingi Tabata jijini Dar es Salaam.


Katika Bonza hilo timu hiyo ya Bongo Movie, ilishindwa kufurukuta katika mechi zote mbili ilizokuwa imepangiwa na kujikuta ikiambulia patupu.

Hadi mwisho wa michuano hiyo timu ya Long Room, iliibuka kidedea na kukabidhiwa set ya Jezi na kleti tatu za bia.

LADY JAYDEE AFANYA KWELI AMSTERDAM



Hapa jide akifanya vitu vyake



KILIMANJARO HOTEL ILIVYONOGA SIKU YA PASAKA

Sikukuu ya pasaka maeneo ya Kilimanjaro Hotel Kempinski kulikuwa na show kali kutoka kwa madj wa Nairobi Kenya, Watu walikuwa wengi pamoja na Celebrity kibao kutoka bongo. Pichani juu kama mnavyowaona madj hao wakiwa kazini. Mpango mzima ulinogaaaaaa!!

Shaa

Seven & Fide

Madame Ritha & Fide





SIKUKUU YA PASAKA NDANI YA COCO BEACH


Sikuu ya Pasaka watu mbalimbali wa Dar walikusanyika sehemu mbalimbali lakini wengine walihudhuria tamasha ambalo liliandaliwa na kampuni ya simu ya Airtel pale maeneo ya Coco Beach. Wasanii walikuwepo na moja kati ya wasanii hao ni Joh Makini kama unavyomuona kwa steji pamoja na Chege na Temba kutoka TMK Wanaume Family

Monday, April 25, 2011

HARUFU YA DAMU



Urafiki uliochipukia hivi karibuni kati ya mastaa maarufu wa filamu Bongo, Wema Sepetu, Rose Ndauka na Jacqueline Pentezel, umezua mjadala huku wadau wakidai eti una harufu ya damu,

Wakizungumza katika nyakati tofauti, baadhi ya mastaa wanaowafahamu vizuri wasanii hao walioanzisha kampuni yao iitwayo JAROWE walidai kuwa, kutokana na tabia zao kuna uwezekano siku moja wakatibuana.
“Mimi nawafahamu vizuri hawa, wote ni moto wa kuotea mbali na kila mmoja yuko juu, hivi ushawahi kuona mafahari wawili wakakaa zizi moja? Nawaambia ipo siku mtasikia kimenuka, sisi tupo,” alisema mmoja wa wasanii aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Jasmine Charles alisema kuwa, yeye alishawahi kuwa na urafiki na wasichana hao kwa nyakati tofauti lakini hawakudumu kutokana na tabia zao.

“Mimi nakwambia wote washawahi kuwa mashoga zangu lakini hatukudumu, sasa leo wameungana, huoni kuna harufu ya damu hapo?” Alihoji mrembo huyo na kuongeza;
“Siwaombei mabaya ila wanatakiwa kuwa makini tu katika kuiendesha kampuni yao kwa nidhamu na kuheshimiana, wamethubutu kufanya jambo la msingi, naamini watafanikiwa.”

Wakizungumzia madai hayo, masistaduu hao ambao tayari wameshaandaa filamu moja walisema kuwa, wanajua mengi yatasemwa lakini wao wako imara na watatimiza kile walicholenga.

“Najua wataongea mengi ila hapa ni kazi tu, sisi wote ni mastaa, tumeamua kuungana ili tutimize ndoto zetu,” alisema Jack.

Naye Wema a.k.a Mrs Diamond alisema: “Wengi hawakutegemea kama sisi tunaweza kufanya kazi pamoja, sasa imekuwa na tunaamini hakuna cha harufu ya damu wala nini, tumedhamiria kuleta mabadiliko.”

WAGONJWA WAVAMIA JIKO LOLIONDO…

Wakati Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapile ‘Babu’ akimalizia mapumziko leo kabla ya kuendelea kutoa tiba ya kikombe, mengi yameibuka katika Kijiji Cha Samunge, Loliondo.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa Wikienda kilichopiga kambi eneo hilo, kituko cha aina yake kilijiri siku ya Ijumaa ambapo baadhi ya wagonjwa wenye nafuu waliokuwa foleni walivuruga utaratibu na kuvamia jikoni kwa Babu na kujichemshia dawa wenyewe.

Chanzo hicho kilidadavua kwamba, wasaidizi wa mchungaji huyo walipigwa na butwaa baada ya kuona watu wakisaka kuni za kuchemshia dawa huku wengine wakienda porini kutafuta mti wa dawa hiyo.
Kilidai kwamba, muda mfupi baadaye, waliokwenda porini kusaka dawa walirejea ambapo waliomba sufuria kwa mmoja wa majirani wa Babu kisha wakawasha moto na kuchemsha dawa waliyokuja nayo.

Ilielezwa kwamba, baada ya kuchemsha dawa walikunywa huku wagonjwa wengine wakivamia na kupata kikombe cha dawa hiyo hadi wakamaliza yote.

Hata hivyo, wagonjwa hao hawakuondoka eneo hilo kwani walielezwa kwamba dawa waliyokunywa haiwezi kuwaponya hadi Babu awape kwa mkono wake mwenyewe.

BONGO INATISHA



Huku Pasaka ikiwa inaishia-ishia zake, matukio kibao ya kutisha yalijiri ndani ya Jiji la Dar huku wengi wakisingizia ni sherehe za sikukuu hiyo.

Katika tukio la kusikitisha, mtu mmoja mwanaume aligongwa na gari na kufa kwa kufumuliwa ubongo alipokuwa akivuka barabara maeneo ya Victoria.

Tukio hilo lilijiri Ijumaa, Aprili 22, mwaka huu ambapo Wakristo duniani kote walikuwa wakikumbuka mateso ya Bwana Yesu Kristo.

Mkononi mtu huyo alikuwa amebeba chipsi kwenye mfuko wa rambo ambazo zilizagaa eneo la tukio mara baada ya ajali hiyo.

MUME AKESHA MLANGO WA GESTI KUMSUBIRI MKEWE
Huko Buguruni, nje ya gesti moja ambayo tunaihifadhi jina, mwanaume mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Baba Sarah, alitumia usiku kucha wa Jumamosi kuamkia Jumapili nje ya mlango wa gesti akidai anamsubiri mkewe, Mama Sarah aliyekuwa na mwanaume ndani ya gesti hiyo.

Hata hivyo, Jumapili, mpaka wahudumu wanafanya usafi kwenye vyumba, mama Sarah hakuwemo ndani na mwanaume huyo aliporudi nyumbani kwake alimkuta mkewe amerudi muda si mrefu.

STEVE NYERERE AKWIDWA
Mchekeshaji maarufu hapa nchini, Steve Mangere ‘Steve Nyerere’, Ijumaa Kuu ilikuwa mbaya kwake baada ya mabaunsa wa Bendi ya Extra Bongo kumkwida na kutaka kumtesa kufuatia kumtuhumu kutaka kuingia bure kwenye onesho la bendi hiyo.

Tukio hilo lilijiri Aprili 22, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Meeda Bar, Sinza ambapo bendi hiyo ilikuwa ikimwaga burudani.
Katika tukio hilo, Steve Nyerere aliyekuwa na msanii mwingine, Salum Mchoma maarufu kama Chiki wakiwa na marafiki zao wawili walifika mlangoni na kutaka kuingia bure, tabia ambayo imeota mizizi kwa masupastaa wa Bongo.

Baada ya wasanii hao kutakiwa kutoa kiingilio, Steve Nyerere alizama mfukoni kwa hasira na kutoa Shilingi za Kibongo 20,000 na kulipa kiingilio cha watu wanne.

Wakati wakiingia, Steve alianza kuwashutumu watu wa getini kwa kumtoza kiingilio huku akiwakejeli kuwa, hawana lolote, kwanza yeye alifika ukumbini hapo kwa kuitwa na bosi wao, Chifu Kiumbe.
Majigambo hayo yalionekana kumkera mmoja wa walinzi wa getini ambaye alimvamia na kumkwida kabla ya kutaka kumshushia kipigo lakini wasamaria wema waliingilia kati na kumtoa nje ya ukumbi mlinzi huyo aliyekuwa mbogo.

Akizungumza na gazeti hili ukumbini hapo, Steve alisema yeye ameitwa ukumbini hapo na Chifu Kiumbe ambaye ni mdau mkubwa wa bendi hiyo lakini anamshangaa mlinzi huyo kujifanya kilimilimi.
“Ole wake wamemkamata, ningemfundisha adabu yule, hanijui mimi. Ningempa pigo moja tu takatifu mwenyewe angemkumbuka mama yake,” alisema Steve kwa kujitapa huku akihema kwa nguvu.

MREMBO AZIMIKA
Katika nderemo za Pasaka, ndani ya Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni, Dar, mrembo mpya wa Bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’ katika safu ya unenguaji, Mariam Sagwa alijikuta akidondoka stejini na kuzimika kwa dakika kadhaa baada ya kupandwa na ‘mzungu’ wakati akinengua.
Tukio hilo lilimkuta Mariam alipokuwa akionesha makeke ya kunengua kionjo cha ‘Ahamada Umelewa’ akilenga kuwapagawisha mashabiki waliokuwa wamefurika ukumbini humo.
Hata hivyo, wanenguaji wenzake walimpiga ‘tafu’ ya kusimama lakini alionekana akiyumbayumba hadi alipotolewa stejini.

FAGASON ABAMBWA
The Big Rapa ndani ya Bendi ya Extra Bongo, Saulo John ‘Fagason’, amejikuta akikosa uhuru alipobananishwa na mchumba wake, Angel Bushuke bila kujali kuwa mzee alikuwa mzigoni.

Tukio hilo lilichukuwa nafasi Ijumaa iliyopita saa tisa usiku katika Ukumbi wa Maeda Sinza Mori, ambapo Bendi ya Extra Bongo ilikuwa ikifanya vitu vyake.
Awali, Fagason alionekana akiinuka kila alipotakiwa kuingia katika nafasi yake ya uimbaji lakini alipomaliza tu kuimba, alilazimika kuelekea pale alipokuwa amekaa mpenzi wake kwani mama alikuwa akimsindikiza kwa macho hatua kwa hatua na kufikia mikao ya ‘kimalavidavi’.

“Mi naona ni haki yake kunibana hivi, kwa sababu ananipenda na mimi nampenda. Pia siku si nyingi tunatarajia kufunga ndoa,” alisema Fagason.

MCHUMBA WA MTU AKUTWA ‘AKIDENDEKA’ HADHARANI
Katika matukio machafu yaliyojiri ndani ya kipindi cha shamrashamra za Pasaka, ‘janki’ mmoja anayechipukia katika ulingo wa filamu za Bongo, Tabasamu Mohamed amekutwa akifanya madudu hadharani na mchumba wa mtu aliyejulikana kwa jina moja la Vumilia kwa kile kilichoonesha kuwa, alikuwa akisaka umaarufu.

Tukio hilo lilinaswa laivu na paparazi wetu Jumamosi iliyopita katika Viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar huku watu wakiwa katika hekaheka za Sikukuu ya Pasaka.

“Siyo kama nimelewa kiviile, ila huyu ni wa kuzugia japo najua ana mchumba wake na mimi pia nina wangu,” alisema Tabasamu.