Social Icons

Saturday, December 24, 2011

TIGO YATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO

Tigo yasaidia wahanga wa mafuriko jijini Dar es Salaam

22 Desemba, 2011. Dar es Salaam. Kampuni ya simu za mkononi Tigo imetoa msaada katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, kwa ajili ya kuwasaidia wananchi waliokumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.

Makakabidhiano hayo yanafanyika leo katika shule ya Sekondari ya Azania, ambayo ni mojawapo ya vituo vilivyoteuliwa na uongozi wa mkoa kwa ajili ya kuweka kambi ya waathirika wa mafuriko hayo.

Msaada huo umekabidhiwa na Mkuu wa biashara na Mauzo wa Tigo. Gaudens Mushi na kupokelewa na Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa.

Katika mkoa wa Dar es Salaam inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 100,000 wameathirika na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Kupitia kitengo chake cha kusaidia jamii Tigo imetoa msaada wa vyakula pamoja na mahitaji mengine muhimu ya kibinadamu.

Meya wa Ilala Jerry Slaa amewaomba watu kuhama katika sehemu za mabondeni “Tunawasihi watu kuhama katika sehemu za mabondeni ili kuepusha matukio ya hatari kama haya. Tumeshapoteza maishakwenye haya maafa , jambo la kusikitisha sana ” alisema
“Kila mmoja anafahamu kuwa mpaka sasa hivi tayari mamia ya watu wamekosa makazi na hawana mahali pa kwenda, Tuna imani kwamba msaada huu utawasaidia kwa kiasi fulani wale ambao wako katika kipindi kigumu kwa sasa,” alisema Gaudens Mushi

Inasemekana kuwa watu kadhaa wamepoteza maisha kutokana na mvua zinazonyesha katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Kutokana na hali hiyo Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam imetenga maeneo maalum ya muda kwa ajili ya kusaidia waathrika wa mafuriko hayo. Maeneo hayo ni Shule ya Azania, Shule ya Msingi Mchikichini, Shule ya Sekondari ya Msimbazi, Shule ya Msingi ya Mzambarauni Ukonga, Shule ya Msingi ya Gilman Rutihinda na Shule ya Sekondari ya Juhudi.


0 comments: