Social Icons

Thursday, October 13, 2011

'MR FLAVOUR ATUA BONGO MCHANA HUU'


KESHO itakuwa patashika ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee, ambapo mashindano ya Bongo Star Search Second Chance 2011, yatakuwa yakifikia ukingoni, huku msanii mkubwa kutoka nchini Nigeria Chinedu Okoli N’Abania ‘Mr Flavour’ ambaye ametua nchini leo hii atapagawisha.

Akizungumza na MATEJA20 Mratibu wa shindano hilo, Rita Paulsen ‘Madam Rita’ alisema kuwa kesho kutakuwa na shoo za aina yake, ambapo msanii kutoka nchini Nigeria Chinedu Okoli N’Abania ‘Mr Flavour’ tayali ameshatua nchini kwaajili ya kutumbuiza katika tamasha hilo.

Usiku wa kesho pia utatawaliwa na wakali wote waliowahi kutikisa mashindano hayo siku za nyuma kama Peter Msechu, Misoji Kwabi, Mariam Mashauri na Jumanne Idd, bila kusahau shoo kutoka kwa washiriki wa shindano hilo.

“Tumejiandaa kadri ya uwezo wetu wote na naamini kutokana na hili mambo yatakuwa mazuri, kwani itakuwa kama nilivyotangaza toka awali ambapo mshindi wa kwanza atapata shilingi Ml. 40 mshindi wa pili ml. 10 na mshindi wa tatu akitoka na shilingi mil 5, kwa hili hakuna longo longo mambo yako safi,”

" Naomba wale wote wanaohitaji tiketi bado zipo na zinapatikana kwenye maduka ya Shee Illusion Mlimani City na Millenium Tower Kijitonyama, Biggy Respect Kariakoo, Steers City Centre, Maduka ya Zizzou Fashion Sinza na Victoria, Beauty Point Shoppers Plaza, Mbalamwezi Beach Club Mikocheni, Manywele Cosmetics Kinondoni, Best Bite, Engine Mbezi Beach na Diamond Jubilee," alisema Madam Rita.

Washiriki wanaoshindania milioni 40 ni Bella Kombo, Haji Ramadhani, Rogers Lucas na Waziri Salum.

1 comments:

rosetarimo said...

nangojea kuona mshindi ni nana?