Social Icons

Monday, October 10, 2011

'KALALA JUNIOR AREJEA TWANGA PEPETA'Kalala Junior akitumbuiza stejini hapo.

Juzikati mwanamuziki wa Bendi ya Mapacha Watatu Kalala Junior, aliibukia katika bendi yake ya zamani ya African Stars International 'Twanga Pepeta' na kujumuika kwa kuimba na wanamuziki hao jambo ambalo lilileta msisimko mkubwa kwa mashabiki wa bendi hiyo na wengine kubaki wakihoji kama msanii huyo atakakua kajiunga na bendi hiyo tena au laa.
Mpango mzima ulikuwa ndani ya Ukumbi wa Mango Garden Kinondo jijini Dar es Salaam.
Kalala Junior akionyesha uwezo wa kukata nyonga kwa mashabiki.
Mwanamuziki wa Twanga Pepeta Saleh Kupaza (kushoto), akiimba wimbo wa Mapenzi hayana kiapo, sambamba na Kalala Junior.
Dogo Rama na Kalala Junior, wakiwajibika jukwaani hapo.
Shaka Zuru, akishindana kuchezea nyuzi za gitaa na Kalala Junior.
Chalz Baba, akimpongeza Kalala Junior kwa ujio wake.
Chalza Baba akimtunza Kalala Junior.
Kalala akiongoza jahazi la Twanga Pepeta kwa 'kurap' Wimbo wa Mapenzi hayana kiapo Ukumbini hapo.
Papa Mathew akimtunza Kalala Junior.
... akimpa heshima zote.
Jojo Jumanne (kushoto), akikung'uta gitaa, huku MCD naye akichalaza Tumba kama kawa.
Kalala akionyesha uwezo zaidi katika gitaa.
Jojo Jumanne ... hashindwi mtu kitu hapa... bhana....
Wanenguaji wa bendi hiyo wakiwajibika.

0 comments: